Friday, January 25, 2013

WAZEE WA UTURUKI WAISUBIRI PRISONS DAR

Wazee wa Uturuki... Nadir Haroub 'Cannavaro'(kushoto) na Nizar Khalfan wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi ya timu yao ya Yanga nchini Uturuki Desemba 31, 2012.

Kutoka kushoto ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Frank Domayo na Simon Msuva. Hapa wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi ya timu yao ya Yanga nchini Uturuki Desemba 31, 2012. 

YANGA iliyopiga kambi ya mazoezi kwa takribani wiki mbili mjini Antalya, Uturuki itaanza mzunguko wa pili dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi itakayochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vinara hao wa VPL wakiongoza kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Azam wanaowafuatia wanaikabili Tanzania Prisons ambayo imetumia dirisha dogo kuongeza wachezaji wawili akiwemo mshambuliaji mkongwe Emmanuel Gabriel.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya. Hivyo kiu ya washabiki ni kutaka kujua nani ataibuka mbabe kati ya timu hizo msimu huu.

Wakati ameingiza wachezaji wawili kwenye dirisha dogo, Kocha wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale amempoteza David Mwantika katika dirisa hilo. Beki huyo ametua katika timu ya Azam.

No comments:

Post a Comment