Thursday, January 31, 2013

GIBBS NJE WIKI 3 ARSENAL IKITOKA SARE YA 2-2 NA LIVERPOOL

Gibbs
Jamie Carragher wa Liverpool akijaribu kumdhibiti Theo Walcott wa Arsenal wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 30, 2013.
Acheni hizo, mkitaka muwe mabondia tujue moja.... Steven Gerrard wa Liverpool akiwatenganisha Olivier Giroud wa Arsenal na Daniel Agger wa Liverpool walipokuwa wakibwatukiana wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 30, 2013.
Olivier Giroud wa Arsenal akijilaumu baada ya kupoteza nafasi ya kufunga dhidi ya Liverpool wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 30, 2013.
Bacary Sagna wa Arsenal na Luis Suarez wa Liverpool wakiwania mpira wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 30, 2013.

Luis Suarez wa Liverpool akiruka juu ya Jordan Henderson wa Liverpool wakati akishangilia kuifungia timu yao goli la pili pamoja na wachezaji wenzao wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England jana Januari 30, 2013.

BEKI wa Arsenal, Kieran Gibbs atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kutokana na maumivu ya paja.

Mlinzi huyo wa England (23) aliondoka akichechemea wakati wa mechi yao ya waliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool na sasa atakosa mechi za Ligi Kuu dhidi ya Stoke na Sunderland, na pengine ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Bayern Munich.

Hakika ni pigo kwetu," alisema kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

"Ni muhimu kwetu kutokana na anavyopanda mbele kushambulia na aina ya mchezo tunaotaka kucheza."

Wenger, ambaye alimuingiza Andre Santos kuchukua nafasi ya Gibbs jana, alisema alifirikia kusajili mchezaji mpya kabla dirisha halijafungwa leo usiku, lakini aliongeza usajili wa mshambuliaji wa Hispania, David Villa, hautafanyika.

Nyota huyo wa Barcelona amekuwa akitakiwa na Wenger lakini dili hilo limekufa na, alipoulizwa kama mpango huo umekufa alijibu: "Ndiyo."

Katika mechi hiyo ya ligi kuu jana usiku kwenye Uwanja wa Emirates, Liverpool walienda wakiongoza kwa magoli 2-0 kutoka kwa Luis Suarez na Jordan Handerson kabla ya Arsenal kucharuka na kutawala kipindi chote cha pili na kusawazisha kupitia kwa Olivier Giroud na Theo Walcott.

No comments:

Post a Comment