Thursday, January 31, 2013

TUMESHINDA KIBAHATI, ASEMA FERGUSON

Sir Alex Ferguson kocha wa Manchester United akiangalia wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England jana Januari 30, 2013.
Wayne Rooney wa Manchester United akifunga goli lao la pili wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England jana Januari 30, 2013.
Wayne Rooney wa Manchester United akifunga goli lao la pili wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England jana Januari 30, 2013.
Wayne Rooney wa Manchester United akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli lao la pili wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England jana Januari 30, 2013.

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema timu yake ilikuwa na bahati kuifunga Southampton katika ushindi wa 2-1, akielezea kiwango cha wageni katika kipindi cha pili kuwa ni bora kabisa kwenye Uwanja wa Old Trafford msimu huu.

Southampton walipata goli la kuongoza kupitia kwa Jay Rodriguez, lakini magoli mawili ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Wayne Rooney yaliwapa ushindi.

"Katika dakika 30 za kwanza tulicheza vyema," Ferguson aliiambia BBC Sport.

"Lakini katika kipindi cha pili Southampton wamecheza vizuri kuliko timu zote zilizokuja hapa msimu huu. Tulikuwa  na bahati kushinda."

Magoli ya Rooney yamefanya jumla ya mabao yake kuwa 12 msimu huu, wakati Shinji Kagawa pia aligongesha nguzo ya goli katika kipindi cha kwanza wakati wenyeji walipozinguza kutoka katika mwanzo mbaya na kufikisha tofauti ya pointi saba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England

Pasi ya nyuma ya Michael Carrick ilishindwa kumfikia David de Gea na Rodriguez akaiba mpira na kufunga kutokea kwenye 'kona ngumu'.

Na katika kipindi cha pili, Southampton waliiweka roho juu timu ya Ferguson wakati wakiishambulia mfululizo safu ya ulinzi ya Man United na De Gea alilazimika kuokoa kiufundi mpira wa 'fri-kiki' kutoka kwa Rickie Lambert.

Ferguson pia alilalamikia hali ya uwanja wao wa Old Trafford wakati Man United walipokuwa wakipata wakati mgumu kupasiana mipira.

"Uwanja ulikuwa mgumu kupasiana. Southampton walikuwa wakishinda kila walipogombea mpira wa 50-50," aliongeza. "Mechi dhidi ya Newcastle na West Brom ziliuua uwanja.

"Tuliumwagilia maji kabla ya mechi lakini ulipokauka katika kipindi cha pili ikawa ngumu kucheza. Walicheza vizuri zaidi yetu na hawakutupa muda wa kukaa na mpira."

No comments:

Post a Comment