Saturday, January 5, 2013

FERGIE: SIHOFII MKATABA WA FERDINAND

Rio Ferdinand

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema "hana presha" kuhusua suala la mkataba wa Rio Ferdinand.

Mkataba wa Ferdinand unamalizika mwisho wa msimu huu, jambo linalomfanya beki huyo kuwa huru hivi sasa kuzungumza na klabu nyingine, au kuondoka bure mwisho wa msimu.
Continue reading the main story   

"Sidhani kama Rio anataka kuondoka na, kama nilivyosema kabla, anaweza kuendelea kucheza," alisema Ferguson kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34.

Mwezi Novemba, beki huyo alisema kwamba hana haraka kuhusu kusaini mkataba mpya.

Kumekuwapo na ripoti kwamba beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England anatakiwa na klabu za Marekani na Mashariki ya Mbali.

Ferdinand amecheza mechi 18 katika ya 30 za United katika michuano yote msimu huu.

Na Ferguson anajiamini kwamba beki huyo anaweza kuendelea kuichezea Manchester kama ataongozwa kwa umakini.

"Sidhani kama ana tatizo la mgongo kama alilokuwa nalo miaka kadhaa iliyopita. Linadhibitika sasa," alisema.

"Hakuna namna kwamba umtarajie acheze kila baada ya siku nne msimu mzima hata hivyo.

"Kupumzika katika muda sahihi kutamsaidia na anafanya kazi kubwa kujiandaa na mechi hivi sasa, kwa kucheza yoga na mambo mengine mengi ili kumsaidia kuongeza muda wa kucheza."

No comments:

Post a Comment