Saturday, January 5, 2013

DJOUROU AJIUNGA HANNOVER KWA MKOPO

Johan Djourou

BEKI wa Arsenal, Johan Djourou ameafiki kujiunga na klabu ya Bundesliga ya Hannover 96 kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswisi (25), amecheza mechi mbili tu msimu huu, akiwa na nahodha wa kikosi cha Arsenal kilichoshinda mechi za Kombe la Ligi dhidi ya Coventry na Reading.

"Kila mmoja hapa Arsenal anapenda kumtakia mema Johan kwa muda akakaokuwa nchini Ujerumani," Arsenal ilisema katika taarifa yake.

Djourou amecheza mechi 144 akiwa na Arsenal tangu alipochezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza dhidi ya Manchester City Oktoba 2004.

Alicheza kwa mkopo pia Birmingham mwaka 2007, ambako alicheza mechi 13.

Djourou ameichezea timu yake ya taifa ya Uswisi zaidi ya mara 30 na alikuwamo katika kikosi kilichocheza fainali za Kombe la Dunia 2006 na Euro 2008.

No comments:

Post a Comment