Saturday, January 5, 2013

DEMBA BA AANZA NA MBILI CHELSEA IKIUA 5-1 KOMBE LA FA.... MAN CITY YAPIGA MTU 3-0... BALOTELLI NDANI

Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea
Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea
Nimekuja kufanya kazi...
Nataka msahau machungu ya kumkosa Drogba
Ba akishangilia
Ba akitupia goli la pili
Hamkukosea kunisajili... Ba akishangilia

Balotelli akishuhudia mechi yao dhidi ya Watford kutokea benchi leo.
MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Demba Ba aliyejiunga jana akitokea Newcastle, ameanza mechi yake ya kwanza na magoli mawili wakati alipoiongoza Chelsea kushinda 5-1 dhidi ya Southampton katika mechi yao ya Kombe la FA iliyochezwa leo.

Mabingwa watetezi licha ya kutawala mechi, walijikuta wakitanguliwa kwa goli la dakika ya 22 lililofungwa na Jay Rodriguez aliyepachika bao lake la tano msimu huu kufuatia pasi kali ya kupenyezewa na Jason Puncheon.

Msenegal huyo aliyekuwa amevaa jezi ya Chelsea kwa mara ya kwanza, aliisawazishia timu yake mpya katika dakika ya 35 akimalizia kuuvusha kwenye mstari mpira ulipigwa na Juam Mata ambao ungeweza kuokolewa na beki wa wenyeji.

Muafrika mwenzake Ba, Victor Moses, raia wa Nigeria, aliifungia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 45 akipiga shuti zuri la mguu wa kushoto kutokea nje ya boksi kufuatia pasi ya nahodha wa kipindi cha kwanza, Ashley Cole.

Beki Branislav Ivanovic aliongeza la tatu katika dakika ya 52, Ba akakamilisha mwanzo wake mzuri kwa kufunga la nne katika dakika ya 61 kabla ya Frank Lampard aliyeingia kutokea benchi kufunga la tano kwa penalti katika dakika ya 83.

Katika mechi nyingine za leo, Man City ambayo ilimuanzisha benchi mshambuliaji mtata Mario Balotelli kabla ya kuingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Edin Dzeko, iliilaza Watford kwa magoli 3-0 yaliyofungwa na Carlos Tevez kwa 'fri-kiki' ya hatari kutoka umbali wa yadi 25 katika dakika ya 25, Gareth Barry (dk. 44) na Marcos Lopes (dk.  90+1).

Tottenham ilishinda kwa magoli 3-0 dhidi ya Coventry yaliyofungwa na Clint Dempsey (dk. 14 na dk. 37) na Gareth Bale (dk. 33).


MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA FA LEO

Southampton 1 - 5 Chelsea

Man City 3 - 0 Watford

Tottenham 3 - 0 Coventry

Wigan 1 - 1 Bournemouth

QPR 1 - 1 West Brom

Southend 2 - 2 Brentford

Aldershot 3 - 1 Rotherham

Aston Villa 2 - 1 Ipswich

Barnsley 1 - 0 Burnley

Blackburn 2 - 0 Bristol City

Bolton 2 - 2 Sunderland

Charlton 0 - 1 Huddersfield

Crawley 1 - 3 Reading

Crystal Palace 0 - 0 Stoke

Derby 5 - 0 Tranmere

Fulham 1 - 1 Blackpool

Hull 1 - 1 Leyton Orient

Leeds United 1 - 1 Birmingham

Leicester 2 - 0 Burton Albion

Luton 1 - 0 Wolves

Macclesfield 2 - 1 Cardiff

Middlesbrough 4 - 1 Hastings Utd

Millwall 1 - 0 Preston

Nottm Forest 2 - 3 Oldham

Oxford Utd 0 - 3 Sheff Utd

Peterborough 0 - 3 Norwich

Sheff Wed 0 - 0 MK Dons

No comments:

Post a Comment