Tuesday, January 22, 2013

FALCAO ACHUKIZWA RIPOTI ZA KUMSINDIKIZA RONALDO

Radamel Falcao

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao amekerwa na uvumi unaomhusisha na mipango ya kutimkia Real Madrid. 

Falcao amekerwa na ripoti kwamba alipata mlo wa jioni na rais wa Real, Florentino Perez kujadili uhamisho wake na ikadaiwa pia kwamba alimsindikiza Cristiano Ronaldo kwenye hafla ya tuzo za Ballon d'Or. 

"Kila kitu ni uongo. Yote yanayoripotiwa kuhusu mimi ni uongo. Kwamba nimekula na Florentino ni uongo. Si kweli kwamba nilisafiri na Cristiano kwenda kwenye tuzo za Golden Ball," alisema Mcolombia huyo. (AS)

No comments:

Post a Comment