Tuesday, January 8, 2013

CASILLAS ALIMPIGIA KURA MOURINHO DHIDI YA KOCHA WAKE WA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA, DEL BOSQUE

Casillas na mwandani wake wakihudhuria tuzo za Ballon d'Or jana

IKER Casillas, nahodha wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, alimpigia kura bosi wa klabu yake Jose Mourinho (pointi 5) dhidi ya Vicente Del Bosque (pointi 3) katika kura zake za tuzo za Ballon d'Or. Chaguo lake la tatu alimpigia Roberto Di Matteo (pointi 1), ambaye aliiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Kwa upande wa tuzo za Mwanasoka Bora, Casillas alimpa Sergio Ramos pointi 5, Cristiano Ronaldo 3 na Xavi 1.

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi alimpa pointi 5 Pep Guardiola, Vicente Del Bosque (3)na Jose Mourinho (1). Katika kura za wachezaji, Messi alimpa Iniesta (5), Xavi (3) na Muargentina mwenzake, Sergio 'Kun' Aguero (1).

Nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Ureno, Bruno Alves ambaye alipiga kura badala ya Ronaldo ambaye alikywa mgonjwa, alimpa pointi 5 Cristiano Ronaldo, Falcao (3) na Van Persie (1). Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella alimpigia Messi (5), Aguero (3) na Falcao (1).

Wakati wa sherehe za Ballon d'Or, Ronaldo alisema kwamba majeraha yalimzui kupiga kura akiwa kama nahodha wa Ureno. "Sikupiga kura. Niliumia mazoezini na tkmu ya taifa ya Ureno na nikarudishwa nyumbani," alifafanua. "Ningempigia nani? Hiyo ni siri yangu," aliongeza.

No comments:

Post a Comment