Tuesday, January 8, 2013

BA AKERWA NA MASWALI MFULULIZO KUHUSU GOTI LAKE

Demba Ba

STRAIKA mpya wa Chelsea, Demba Ba amesisitiza kwamba idadi ya mechi alizocheza kwenye Ligi Kuu ya England inathibitisha kwamba hana tatizo kwenye goti lake.

Stoke City walikaribia kumsajili Ba Januari 2011 lakini dili hilo lilipeperuka baada ya kushindwa vipimo vya afya huku kocha Tony Pulis akiwaonya West Ham waliokubali kumsajili hivyo hivyo kwamba goti la Ba ni bomu linalohesabu dakika kabla ya kulipuka.

Ba ambaye alijiunga na West Ham United, kabla ya kutisha tena akiwa na Newcastle United, amesema Chelsea hawahofii suala lake la uzima wa muda mrefu ndiyo maana wakamsajili wiki iliyopita.

"Goti langu la kushoto? Hakika hakuna tatizo lolote kwa Chelsea," straika huyo aliliambia gazeti la L'Equipe.

"Sipendi kuzungumzia kuhusu hilo, lakini angalia tu idadi ya mechi nilizocheza tangu nilipotua England (mechi 65 za Ligi Kuu). Jibu nadhani linatosha kumridhisha kila mmoja."

No comments:

Post a Comment