Tuesday, January 8, 2013

MOURINHO KUMTUPA TENA BENCHI CASILLAS PALE ADAN ATAKAPOMALIZA KUTUMIKIA ADHABU YA KADI NYEKUNDU

Casillas (kulia) akimliwaza Adan baada ya kula 'red' huku Mourinho akiwa kushoto

IKER Casillas atarejea langoni mwa Real Madrid katika mechi ya kesho Jumatano ya Kombe la Mfalme dhidi ya Celta Vigo na ya ligi Jumamosi dhidi ya Osasuna. Lakini kurejea kwake kwenye kikosi cha kwanza ni kwa muda mfupi tu. Jose Mourinho tayari ameamua kwamba Antonio Adan atarejea katika kikosi cha kwanza katika mechi itakayofuata dhidi ya Valencia.

Mou hakutishwa na miluzi na kuzomewa na mashabiki wa Real kwenye uwanja wao wa Bernabeu wakati 'skrini' kubwa ya uwanjani ilipoonyesha jina la Adan kuwa ndiye atakayesimama langoni Jumapili, jambo lililothibitisha mvutano mkubwa baina ya kocha huyo Mreno na mashabiki "damu" wa Madrid. Mourinho anaamini katika anachokifanya na ataendelea na msimamo wake wa kufanya maamuzi anayoona yana manufaa kwa timu bila ya kujali yanapokewaje.

Machoni mwa 'Special One', hakuna anachoweza kukifanya kama watu hawataki kuamini kwamba tatizo lake na Casillas ni kuhusu kiwango tu na nahodha huyo. Hii si vita ya nani zaidi, alidai: anachotaka ni Iker kuzuia mipira isitinge wavuni, lakini kipa huyo hafanyi hivyo – aua angalau alivyokuwa akifanya zamani. Kocha huyo amezidi kuhofia udhaifu unaoongezeka wa Casillas linapobaki suala la kubaki yeye na mshambuliaji tu, jambo ambalo alikuwa akisifika nalo sana. Kutokana na hivyo, Mourinho hamchezeshi Adan kama njia ya kumtumia ujumbe Casillas ama mashabiki: anaona uwezo wake umeshuka.

No comments:

Post a Comment