Monday, January 7, 2013

BOATENG ALIKOSEA KUTOKA UWANJANI - BLATTER

Kevin-Prince Boateng wa AC Milan akiwa amevaa jezi ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya mechi yao ya Serie A dhidi ya Siena kwenye Uwanja wa San Siro mjini Milan, Italia jana Januari 6, 2013.

Kevin-Prince Boateng wa AC Milan akiwa amevaa jezi ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya mechi yao ya Serie A dhidi ya Siena kwenye Uwanja wa San Siro mjini Milan, Italia jana Januari 6, 2013.

Kevin-Prince Boateng (kulia) na wachezaji wenzake wa AC Milan wakiwa wamevaa jezi za kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya mechi yao ya Serie A dhidi ya Siena kwenye Uwanja wa San Siro mjini Milan, Italia jana Januari 6, 2013.

RAIS wa FIFA, Sepp Blatter amesema Kevin-Prince Boateng alikosea kutoka nje ya uwanja baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi katika mechi yao ya kirafiki wiki iliyopita.

Kiungo huyo AC Milan aliamua kutoka nje ya uwanja katika mechi yao ya kirafiki dhidi yatimu ya daraja la chini ya Pro Patria, baada ya kikundi kidogo cha mashabiki wa timu mwenyeji kumfanyia vitendo vya kibaguzi nyota huyo wa Ghana na baadhi ya wachezaji wenzake.

“Kutoka nje ya uwanja? Hapana, sidhani kama hili ni suluhisho," Blatter aliwaambia waandishi wa habari Dubai. "Lakini shirikisho la soka la Italia bado halijawasilisha FIFA ripoti ya nini hasa kilichotokea. Sidhani kama unaweza kukimbia, kwa sababu unaweza kuifanya sababu ya kukimbia mechi ukiona mmeshafungwa.

"Jambo hili ni suala linalogusa sana, lakini narudia tena kwamba ubaguzi haukubaliki hata kidogo kwenye viwanja vya soka; na lazima tupambane navyo. Suluhisho pekee ni kutoa adhabu kali sana - na adhabu ziwe kukatwa pointi au kitu kama hicho."

Klabu ya AC Milan ilionyesha sapoti kwa Boateng kabla ya mechi ya jana waliyoshinda 2-1 dhidi ya Siena, ambapo kikosi kizima kilivaa fulana zilizoandikwa 'AC Milan dhidi ya ubaguzi'.

No comments:

Post a Comment