Thursday, January 24, 2013

SWANSEA YAITOA CHELSEA KOMBE LA LIGI... HAZARD AMPIGA TEKE MUOKOTA MIPIRA

Eden Hazard (kulia) wa Chelsea akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke kijana anayeokota mipira wakati wa mechi yao ya marudiano ya Kombe la Ligi (Capital One Cup) dhidi ya Swansea jana usiku.
Demba Ba (kushoto) wa Chelsea akipiga shuti dhidi ya Ashley Williams wa Swansea City wakati wa mechi yao ya marudiano ya Kombe la Ligi (Capital One Cup) dhidi ya Swansea kwenye Uwanja wa Liberty, mjini Swansea nchini Wales jana usiku Januari 23, 2013.Timu hizo zilitoka sare ya 0-0. Chelsea wqakatolewa kwa jumla ya magoli 2-0.

SWANSEA City wametinga katika fainali yao ya kwanza ya Kombe la Ligi baada ya kuwashikilia Chelsea waliobaki 10 uwanjani katika sare ya bila goli kwenye nusu fainali ya utata katika Uwanja wa Liberty Stadium.

Matokea ya jumla yaliwapa Swansea ushindi wa 2-0, lakini yalisaidiwa kidogo mno na kutolewa na kwa kadi nyekundu kwa kiungo wa Chelsea, Eden Hazard ambaye alimpiga teke mtoto anayeokota mipira.

Kiungo huyo Mbelgiji alitolewa katika dakika ya 80 baada ya kutukio hilo lililotokea nyuma ya goli la wenyeji.

Swansea sasa watacheza dhidi ya timu ya daraja la nne ya Bradford katika fainali kwenye Uwanja wa Wembley.

Kadi nyekundu ya Hazard ilikuja baada ya kuvutana na muokota mipira, ambaye alikuwa akichelewa kurejesha mipira uwanjani. Alionekana kuulalia mpira na picha za TV zilionyesha Hazard akimpiga teke.

Benitez alianza kwa kumpumzisha Fernando Torres benchi na kumuanzisha Demba Ba katika safu ya mashambulizi lakini hapakuwa na goli jana.

Katika ratiba nyingine iliyotoa matokeo ya ajabu, kocha wa Bradford, Phil Parkinson ana shaka kwamba hakuna tena timu ya kutoka ligi daraja la nne itakayoweza kufika fainali ya kombe la ligi.

Parkinson aliishuhudia timu yake ikiing'oa Aston Villa kwa jumla ya magoli 4-3 baada ya kulala 2-1 ugenini Villa Park juzi usiku na kutinga fainali ya Capital One Cup itakayochezwa mwezi ujao.

Alisema: "Itakuwa ngumu sana kwa tim,u nyingine kurudia mafanikio haya tena.

"Tulipitia njia ngumu sana. Si dhidi ya timu za Ligi Kuu tu, bali mechi ngumu dhidi ya Notts County na Watford pia."

Bradford walienda kucheza mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Villa Park wakiwa mbele kwa ushindi wa 3-1 walioupata katika mechi yao ya awali, lakini Christian Benteke alipunguza tofauti hiyo ya magoli kwa kuifungia Villa.

James Hanson alifunga kwa kichwa kuisawazishia Bradford kabla ya Andreas Weimann kuifungia Villa goli la pili katika dakika za lala salama.

No comments:

Post a Comment