Wednesday, January 23, 2013

WENGER ANA PAUNDI MILIONI 40 ZA KUSAJILI JANUARI

Arsene Wenger

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ana paundi milioni 40 kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya katika kipindi hiki cha Januari.

Na Mfaransa huyo amesema wanafanya kazi usiku kucha wakijaribu kusajili nyota wapya kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Kocha huyo alikataa kutaja majina ya wachezaji wanaowafukuzia, lakini bado ana matumaini kwamba wataimarisha kikosi chao katika siku zijazozo.

"Ndio [bado nahitaji kusajili wachezaji wawili]. Tunafanya kazi kwa bidii sana katika jambo hilo," alisema Wenger. "Bei si kinachojalisha, ni ubora tu.

"Sitataja majina yoyote. Sitaki kuzungumzia mambo yanayozagaa katika uvumi kwa sababu jambo hilo litaziweka timu zao katika nafasi mbaya. Na mchezaji pia.

"Unapaswa kuheshimu kwamba wachezaji wana mikataba huko waliko, anacheza na kwa kuwa dili halijkamilika kwa yeyote ni vyema kutolizungumzia kwa sababu haisaidii. Analazimika kuendelea kucheza huko aliko."

No comments:

Post a Comment