Tuesday, January 29, 2013

BALOTELLI AANZA KUHAMISHA VITU VYAKE


MARIO Balotelli ameanza kufungasha virago vyake Manchester City.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limesema Balotelli huenda hatimaye sasa akahama kutoka Manchester City wiki hii baada ya miamba ya soka ya Italia, AC Milan kuanza mazungumzo rasmi jana na mabingwa hao wa England kuhusu uhamisho unaotajwa kugharimu paundi milioni 24 kwa ajili ya mshambuliaji huyo mtata.

Balotelli alionekana akibeba baadhi ya vitu vyake kutoka katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo jana kabla ya kwenda kuungana na wachezaji wenzake mjini London kwa ajili ya mechi yao ya leo dhidi ya QPR kwenye Uwanja wa Loftus Road.

Mapema jana Jumatatu, kocha Brian Kidd alimuomba mshambuliaji huyo amsainie kijitabu chake cha kumbukumbu, jambo ambalo lilitafsiriwa kama ishara kwamba muda wa Balotelli klabuni Manchester umefikia tamati.

No comments:

Post a Comment