Tuesday, January 29, 2013

PHIL JONES: NATAKA KUCHEZA BEKI WA KATI

Phil Jones

BEKI wa Manchester United, Phil Jones anajiona kama beki wa kati.

Uwezo wa Jones wa kucheza nafasi tofauti uwanjani umemfanya atumiwe na kocha Sir Alex Ferguson kama beki wa kulia, kiungo na beki wa kati tangu alipotua akitokea Blackburn.

"Nimekuwa nikisisitiza kwamba nafasi ya beki wa kati ndipo mahala ninapojisikia huru zaidi," alisema.

"Nauelewa na nausoma mchezo vyema nikiwa pale. Nitacheza kokote ninakoambiwa, lakini hapatakuwa na shida kucheza pamoja na Chris (Smalling) katika ulinzi wa kati.

"Tumekuwa tukicheza pamoja kama mabeki wa kati katika timu ya taifa ya vijana ya U-21 ya England, tunafahamiana kimchezo na tumezoeana vyema."

No comments:

Post a Comment