Tuesday, January 29, 2013

BALOTELLI AAFIKI MIAKA MINNE NA NUSU AC MILAN

Super Mario

AC Milan wameafiki dili la kumsajili straika wa Manchester City, Mario Balotelli kwa mkataba wa miaka minne na nusu, mkurugenzi wa klabu hiyo ya Italia, Umberto Gandini, amethibitisha.

Straika wa zamani wa Inter Milan, Balotelli (22) atafanyiwa vipimo vya afya mjini Milan Jumatano kabla ya kusaini mkataba wake.

Ada ya awali ya uhamisho inaaminika kuwa ni paundi milioni 19 ambayo inasemekana imeshalipwa na huenda ikaongezeka kufikia paundi milioni 22.

No comments:

Post a Comment