Wednesday, January 2, 2013

BABA WA SAJUKI ATAKA MWANAWE AKAZIKWE SONGEA.... TAZAMA NA MAPICHA YA MAREHEMU ENZI ZA UHAI WAKE... HIVI KARIBUNI ALIANGUKA AKIWA JUKWAANI JIJINI ARUSHA BAADA YA KUISHIWA NGUVU NA KUMWAMBIA MWANDISHI: "HALI YANGU SI NZURI KABISA...NAUMWA SANA!"

Sajuki enzi za uhai wake. Hapa ni kabla hajaanza kusumbuliwa na maradhi.
Baba yake Sajuki, Mzee Kilowoko akiwa kwenye msiba wa mwanawe huyo uliopo Tabata jijini Dar es Salaam leo Januari 2, 2013.
Wastara. Mke wa Sajuki ambaye pia ni msanii wa filamu.

Marehemu Sajuki... hapa ni siku aliyoishiwa nguvu jukwaani Arusha na kuanguka.

Maskini Sajuki... hapa ni enzi zake akiwa hai akifarijiwa na wenzake baada ya kushiwa nguvu jukwaani wakati wakiwa Arusha hivi karibuni.  

Sajuki enzi zake akiwa na mkewe Wastara.



Wastara... mke wa Sajuki alitebaki mkiwa.

Sajuki... hapa ni enzi zake akiwa hai baada ya kuugua na kupata matibabu India kabla ya kurejea nchini.

Baba wa msanii Juma Kilowoko "Sajuki", anataka mwanawe akazikwe kwao mkoani Songea na siyo jijini Dar es Salaam, imefahamika.

Akizungumza leo na kituo cha redio cha East Africa, baba yake Sajuki alisema kuwa yeye na familia yake wanataka kwenda kumzika Sajuki Songea kwani ndiko nyumbani kwao.


"Nia yetu ni kwenda kumzika Songea," amesema mzazi huyo wa Sajuki. Kwa sasa, shughuli za msiba huo Tabata.


Sajuki amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na kuacha majonzi makubwa kwa mashabiki wake wanaokumbuka namna alivyoimarika afya yake kabla ya kudondoka jukwaani hivi karibuni wakati akiwa jijini Arusha..

Msanii huyo alikuwa amelazwa Muhimbili tangu wiki iliyopita kutokana na matatizo ya tumbo na pumu na kuwa katika wodi ya wagonjwa mahututi huku akipumulia mashine.

Taarifa za ndugu wa marehemu zinaeleza kuwa alifariki leo (Januari 2, 2013) mishale ya saa 1:00 asubuhi. Kabla ya kufariki kwake, kulikuwa na mpango wa kumsafirisha tena kwenda kutibiwa nchini India, mahala alikowahi kupelekwa awali na kurejea nchini akiwa katika hali ya unafuu mkubwa.

Wiki iliyopita, mashabiki wa filamu za Kibongo walipata bahati ya kumuona Sajuki akizungumza kwa mara ya mwisho kupitia kipindi cha Mikasi kinachorushwa kila Jumatatu katika kituo cha luninga cha Channel 5 ambapo, marehemu alizungumza mengi wakati akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salam Jabir.

KUANGUKA ARUSHA
Baada ya kuchangiwa na Watanzania wengi wenye mapenzi naye wakiwamo wabunge kama Zitto Kabwe, Halima Mdee, Ester Bulaya na Iddi Azzan na kwenda kutibiwa India, Sajuki aliandaa maonyesho kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania kwa kumsaidia kupata matibabu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua na pia kupata fedha za kumrejesha India kwa matibabu.


Alifanya maonyesho hayo katika miji ya Iringa na baadaye Arusha ambako alianguka jukwaani baada ya kuishiwa nguvu.

Onyesho hilo liliwahusisha pia wasanii wengine kadhaa nyota wa filamu na muziki wa kizazi kipya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Sajuki alipopanda jukwaani kuwasalimia mashabiki wake, alifanikiwa kutamka neno moja tu "aghhhhh" na kisha akaanza kudondoka ghafla kabla ya kudakwa na wasanii wenzake waliokuwa jirani yake.

Akizungumza baada ya kuondoshwa jukwaani, Sajuki alisema hali yake kiafya siyo nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.


"Hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri," alisema Sajuki.

No comments:

Post a Comment