Wednesday, January 9, 2013

BEKI AMBAYE BADO TEGEMEO QPR ATEULIWA KOCHA MPYA LIGI KUU YA MAREKANI

Ryan Nelsen wa QPR akiwa uwanjani wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England Novemba 24, 2012 
Ryan Nelsen wa QPR akimiliki mpira dhidi ya Fernando Torres wa Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Januari 2, 2013.
Ryan Nelsen wa QPR na Olivier Giroud wa Arsenal wakiwania mpira wa kichwa wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Oktoba 27, 2012.

Ryan Nelsen wa QPR akimbana Oscar wa Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Januari 2, 2013.


BEKI wa QPR, Ryan Nelsen ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Ligi kuu ya Marekani ya Toronto FC.

Nelsen (35) bado ni nguzo ya ulinzi katika kikosi cha QPR msimu huu, akicheza mechi 21 katika michuano yote tangu alipojiunga nayo Juni.

Mkataba wa Nelsen na QPR unamalizika Juni 30 lakini ameomba kufanya mazungumzo na kocha wa QPR, Harry Redknapp kujadili ni lini atahamia Canada yaliyoko maskani ya Totonto FC.

QPR wamethibitisha kwamba Nelsen atakuwamo kwenye kikosi chao kitakachocheza Jumamosi dhidi ya Tottenham.

Klabu inayoshiriki ligi kuu ya MLS ya Toronto FC, inamtaka Nelsen aanze kuifundisha timu yao kwa ajili ya msimu mpya utakaoanza Machi, lakini QPR huenda wakasisitiza abaki hadi mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya England mwezi Mei.

"Nimezungumza mara kadhaa na Harry na (mmiliki wa klabu) Tony Fernandes," mchezaji huyo raia wa New Zealand alisema.

"Wamekuwa waelewa sana katika suala langu.

"wanafahamu ninapocheza hivi sasa nacheza kama nina magoti ya kioo na enka za vioo. Ninapata shida kidogo.

"Wanajua kwamba niko ukingoni lakini pia wanajua hali waliyonayo sasa katika ligi. It is a major predicament.

"QPR watapenda niendelee kucheza lakini itabidi tukae chini tuzungumze. Kama tutashinda mechi tano mfululizo, hiyo itakuwa safi.

"Nadhani kisha hapo tutapeana mikono na kuachana lakini tutazungumza ktuone itakuwaje."

Nelsen, ambaye aliiwakilisha nchi yake katika fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, alicheza kwa kiwango cha juu wakati alipocheza soka kwenye Ligi ya MLS akiwa na klabu ya DC United kabla ya kuhamia Blackburn mwaka 2005.

Pia alicheza kwa muda mfupi katika klabu ya Tottenham kabla ya kuhamia QPR.

Wakati kuondoka kwa Nelsen kunategemea mafanikio ya Redknapp katika dirisa la usajili la Januari wakati akijaribu kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Mazungumzo zaidi baina ya pande hizo yatafuata siku zijazo.

No comments:

Post a Comment