Thursday, January 24, 2013

ARSENAL YAPATA USHINDI WA KWANZA 2013... YAUA WEST HAM 5-1

Walcott akifunga goli la nne

Olivier Giroud (kulia) akishangilia goli la pili alilopikiwa na Theo Walcott (juu) pamoja na Per Mertesacker

Lukas Podolski Ikulia) akishangilia goli la kwanza alilofunga pamoja na Theo Walcott

ARSENAL ilicheza kwa kiwango cha juu na kupata ushindi wao wa kwanza mwaka 2013 kwa staili ya aina yake baada ya kuisambaratisha West Ham kwa magoli 5-1 jana usiku.

Lakini mechi hiyo iliyojaa burudani, iliathiriwa na kuumia kwa mchezaji wa West Ham, Dan Potts, aliyezimia uwanjani.

Jack Collison aliifungia West Ham goli la kuongoza kwa shuti zuri la nje ya boksi lakini Lukas Podolski alisawazishwa kwa goli kali zaidi ya hilo na tangu wakati huo Arsenal wakatawala mechi.

Olivier Giroud alifunga la pili na Santi Cazorla akatupia la tatu kwa kisigino na kufanya matokeo yawe 3-1. Theo Walcott kisha akafunga la nne kwa shambulizi la kustukiza kabla ya Giroud kufunga la tano.

Kulikuwa na hofu kwa West Ham kuelekea mwishoni mwa kipindi cha pili kufuatia mchezaji wao mwenye umri wa miaka 18 aliyeingia kutokea benchi kuhitaji matibabu ya muda mrefu uwanjani kabla ya kutolewa kwa machela kukimbizwa hospitali.

Arsenal wamebaki wa sita katika msimamo lakini wamepunguza pengo la pointi dhidi ya Tottenham iliyo katika nafasi ya nne kufikia pointi nne, wakati West Ham wako katika nafasi ya 12.

Aprili 2007, West Ham walikuwa ndiyo timu ya kwanza kuifunga Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates baada ya kuhamia wakitokea katika uwanja wao wa zamani wa Highbury kupitia kwa goli la dakika za lala salama kutoka kwa Bobby Zamora lililowapa ushindi wa 1-0.

No comments:

Post a Comment