Wednesday, October 31, 2012

KOCHA STEWART HALL AWASILI DAR LEO... AITAKA AZAM ISHINDE KILA MECHI... KUTAMBULISHWA KESHO

Kocha Muingereza Stewart Hall akivishwa mataji baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo

Kocha Muingereza Stewart Hall akipozi kwa picha baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo

Mashabiki wa Azam wakipiga ngoma na kupuliza vuvuzela wakati wa mapokezi ya kocha Muingereza Stewart Hall kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo


KOCHA Muingereza Stewart Hall ametua jijini Dar es Salaam usiku huu huku akiitaka Azam kushinda kila mechi baada ya kurejea kuifundisha timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili.

Hall amerejea katika klabu yake ya zamani ya Azam baada klabu aliyokuwa akiifundisha Sofapaka ya Kenya inayomilikiwa na tajiri, Papaa Kalekwa, kukiri kwamba haiwezi kupambana na kampuni kubwa ya Azam ambayo imeahidi kumpa mshahara mara mbili ya waliokuwa wakimlipa Wakenya hao.

Mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakipuliza mavuvuzela na kupiga ngoma, waliimba nyimbo mbalimbali ukiwamo uliosema "Hall amerejea, homa na presha za Simba na Yanga ziko juu."

Baada ya kutua kocha huyo, alivishwa mataji ya maua na viongozi wa Azam waliokuwapo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
kwa ajili ya kumpokea.

"Nimejisikia vizuri kwa mapokezi haya mazuri. Naahidi kufanya mazuri. Nataka Azam ishinde kila mechi. Mambo yataanza kesho," alisema Hall ambaye aliondoka katika klabu hiyo baada kutofautiana na uongozi kufuatia kumchezesha winga Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) dhidi ya Yanga, siku chache baada ya winga huyo kupigwa picha akiibusu logo ya jezi ya klabu yake ya zamani ya Yanga.

Uongozi wa Azam ulisema kwamba utafanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kesho kwa ajili ya kumtambulisha kocha huyo aliyeifundisha kimafanikio timu hiyo kwa kuiwezesha kumaliza ikiwa ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita na pia kuifikisha katika fainali ya Kombe la Kagame katika msimu wake wa kwanza kushiriki. Ilifungwa 2-0 na Yanga katika fainali ya Kagame.

Azam iliyomtimua kocha wake aliyemrithi Hall, Mserbia Boris Bunjak, baada ya timu kuangukia katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu, kesho itacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

DIAMOND, RECHO KUTUMBUIZA REDDS MISS TANZANIA... VIINGILIO VYATANGAZWA

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali ya shindano la taifa la Redds Miss Tanzania zitakazofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali ya shindano la taifa la Redds Miss Tanzania zitakazofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali ya shindano la taifa la Redds Miss Tanzania zitakazofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali ya shindano la taifa la Redds Miss Tanzania zitakazofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, Rachel na Wanne Star, ni miongoni wasanii watakaosindikiza fainali za shindano la urembo la Redd's Miss Tanzania 2012 kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam Jumamosi.

Vimwana 30 watachuana katika kuwania kurithi mikoba ya Miss Tanzania wa sasa, Salha Israel.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga, alisema maandalizi yako katika hatua za mwisho kwa ajili ya kumsaka mwakilishi huyo wa nchi katika fainali za urembo za dunia, Miss World 2013.

Lundenga alisema tiketi kwaajili ya shindano hilo zipo tayari na zipo kwa idadi maalum na leo hii zimeanza kuuzwa katika vituo vilivyopendekezwa kulingana na maoni ya wadau.

"Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha Sh. laki moja (100,000) za Kitanzania," alisema.

Alisema wanatarajia ushindani mkali hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo wao ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini.

Alivitaja vituo vilivyoanza kuuza tiketi leo kuwa Stears Samora,
Regency Park Hotel, Rose Garden Mikocheni, Share Illusion-Mlimani City, Giraffe Hotel, Ubungo Plaza na ofisi za Lino na City Sports Lounge iliyopo Posta Mpya mkabala na Mnara wa Askari.

"Nitoe rai kwa wapenzi wote, ni vyema wapate tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu kuna kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali," alisema Lundenga.

Alisema warembo watano tayari wameingia katika Top 15 baada ya kushinda mataji madogo. Aliwataja kuwa ni Lucy Stephano aliyetwaa taji dogo la Miss Photogenic, Magdalena Roy (Miss Top Model), Mary Chizi (Miss Top Sport Woman), Babylove Kalala (Miss Talent) na Happiness Daniel aliyetwaa taji la Miss Personality baada ya kupigiwa kura na warembo wenzake.

"Mwisho napenda kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha Redds Original, Star TV na Giraffe Hotel," alisema Lundenga.     

Mshindi wa taji la mwaka huu atapewa gari, ambalo litatambulishwa siku ya onyesho na fedha taslimu Sh. milioni 8.

YANGA YAIVUTA MKIA SIMBA KILELENI, YONDANI AREJEA UWANJANI KWA MARA YA KWANZA TANGU ALIPOUMIZWA NA BOBAN

Chezea mimi wewe?...... Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la pili wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo jioni. Yanga ilishinda 3-0.
Simon Msuva wa Yanga (kushoto) akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Mgambo JKT wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Tanzania bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

YANGA iliyokuwa na mwanzo mbaya wa msimu, hatimaye imeifikia Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Mgambo JKT, huku Wekundu wa Msimbazi waking'ang'aniwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya timu ya mkiani ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jioni ya leo. 


Ushindi huo unamaanisha kwamba Yanga sasa imelingana pointi 23 na Simba kileleni baada ya mechi 11. Hata hivyo, Simba yenye wastani wa magoli 12, inaendelea kuongoza ligi kwa wastani wa goli moja zaidi ya Yanga yenye wastani wa magoli 11. Simba imefunga magoli 20 na kufungwa 8 wakati Yanga imefunga magoli 21 na kufungwa 10.

Yanga ilianza kuhesabu goli la kwanza katika dakika ya pili tu ya mchezo kupitia kwa beki wake wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyefunga kwa kichwa kufuatia mpira wa 'fri-kiki' uliopigwa na kiungo Haruna Niyonzima.


Mshambuliaji Didier Kavumbagu aliifungia Yanga goli la pili katika dakika ya 39 kufuatia krosi ya Hamis Kiiza na Jerry Tegete akakamilisha ushindi wa kujiamini wa timu yake wakati alipofunga goli la tatu katika dakika ya 79 kufuatia pasi ya Oscar Joshua.

Ulikuwa ni ushindi wa saba katika mechi 11 kwa Yanga na kuwasahaulisha mashabiki wao mwanzo mbaya wa msimu uliowafanya wamfukuze kocha Mbelgiji Tom Saintfiet aliyedumu nao kwa siku 80 tu huku akiwa ameshawapa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Yanga pia ilifurahia kurejea kwa beki wake wa kati, Kelvin Yondani, aliyecheza kwa mara ya kwanza tangu aliponusurika kuumia vibaya zaidi katika rafu mbaya ya "vunja mifupa" aliyochezewa na kiungo Haruna Moshi 'Boban' wa Simba katika mechi ya watani wa jadi Oktoba 3. Aliingia katika dakika ya 46 akichukua nafasi ya beki veterani wa kulia, Shadrack Nsajigwa.   

Mambo hayakuwa mazuri kwa mabingwa Simba ambao walitanguliwa kwa goli la dakika ya 33 kutoka kwa Mokili Lambo, aliyekuwa ameingia uwanjani dakika 5 tu zilizopita kuchukua nafasi ya John Bosco aliyepumzishwa katika dakika ya 28.

Simba walirejea kipindi cha pili wakiwa nyuma kwa goli 1-0 kabla ya kiungo wao aliye katika kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu Amri Kiemba kuwasazishia katika dakika ya 57 akimalizia kona iliyochongwa na Emmanuel Okwi.


Ilikuwa ni sare ya 5 katika mechi 7 zilizopita za Simba baada ya kushinda zote nne za kwanza mfululizo, wakati Polisi ilipata pointi yao ya tatu kutokana na sare tatu huku ikiendelea kubaki mkiani mwa ligi ikiwa haina ushindi baada ya mechi 11. Imefungwa mechi 8.


Sare nyingine katika mechi za ugenini, ilionekana kumchanganya kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic ambaye alidai kwamba refa Jacob Ondongo kutoka Mara alichezesha vibaya na kwamba alionekana kuipendelea timu mwenyeji.


Kocha msaidizi wa Polisi, Ally Jangalu aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri akisema walikuwa na makosa katika upande wa ufungaji lakini wamerekebisha kiwango tangu walipocheza dhidi ya Ruvu Shootings ambapo walilala 2-1 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.


Mgambo ambao waliwashikilia Simba katika sare ya kustusha mkoani Tanga iliyochangia kusimamishwa kwa kiungo wa Wekundu, Haruna Moshi 'Boban', walijikuta wakimaliza wakiwa 10 uwanjani baada ya beki wao Salum Mlima kumchezea rafu beki wa Yanga, Mbuyu Twite katika dakika ya 85 na kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro.


Coastal Union ya Tanga iliyo katika nafasi ya tatu itajaribu kuitetea nafasi yake wakati itakapocheza ugenini dhidi ya Azam iliyo katika nafasi ya nne kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kesho.



Vikosi kwenye Uwanja wa Taifa vilikuwa:

Yanga: 
Ally Mustapha 'Barthez', Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Athumani Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo/ Nurdin Bakari (dk.76), Didier Kavumbagu/ Jerry Tegete (dk.68), Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.

Mgambo JKT:
Godson Mmasa, Salum Mlima, Yasin Awadh, Salum Kipanga, Bakari Mtama, Ramadhan Malima, Chande Maguja, Issa Kanduli/ Nassor Gumbo (dk.59), Fully Maganga na Juma Mwinyimvua/ Omary Matwiko (dk.76).


Vikosi kwenye Uwanja wa Jamhuri vilikuwa:
 
Polisi Morogoro:
Aghaton Mkwando, Nahoda Bakari, John Bosco/ Mokili Lambo (dk.28), Noel Msakwa, Hamis Mamiwa, Abdallah Mfuko, Bantu Admin, Maige Pascal, Ally Shomary, Malimi Busungu, Nicholaus Kabipe.

Simba:
Juma Kaseja,  Nassor Masoud 'Chollo', Amir Maftah, Pascal Ochieng, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.        

MTANZANIA APIGWA TKO PAMBANO LA KUTANGAZA AMANI AFGHANISTAN

Bingwa wa dunia wa taji la Mabara la WBO, Hamid Rahimi akishangilia ushindi baada ya kumpiga Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Bingwa wa dunia wa taji la Mabara la WBO, Hamid Rahimi akishangilia ushindi baada ya kumpiga Said Mbelwa wa Tanzania mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi (kulia) akizichapa na Said Mbelwa (kushoto) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi (kulia) akizichapa na Said Mbelwa (kushoto) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi (kushoto) akionyeshana ubabe na Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
      

KABUL, Afghanistan
MASHABIKI waliojaa furaha wa mjini Kabul walivamia ulingo kushangilia ushindi katika pambano la kwanza la ngumi za kulipwa nchini Afghanistan, baada ya Hamid Rahimi kumpiga Mtanzania Said Mbelwa katika raundi ya saba.

Bondia wa Afghan, Rahimi alimdunda Mbelwa jana jioni na kutwaa mkanda wa ubingwa wa Mabara wa WBO wa uzito wa kati katika pambano lililopewa jina la "Pigana kwa Ajili ya Amani" katika mji ambao unafahamika zaidi kwa vishindo vya milio ya risasi badala ya masumbwi ya 'uppercuts' na 'jabs'.

Waandaaji wamelenga kutumia pambano hilo, ambalo lilihudhuriwa na mashabiki 1,500 waliolipa kiingilio cha angalau dola 100 (Sh. 156,000) ambazo ni zaidi ya mshahara wa mwezi mzima kwa raia wengi wa Afghan, kwa ajili ya kupromoti michezo kama mbinu ya kuwaunganisha Waafghanistan baada ya miongo kadhaa ya vita.

"Pambano hili litatoa somo kwa Wataliban na vikundi vingine vinavyopingana na serikali kuacha kupambana kwa silaha  na kwamba wanaweza kupambana kusaka uongozi bila ya uhalifu," alisema Mohammad Asif Sahibi (28) wakati akishuhudia pambano hilo.

Pambano la jana, ambalo kila ngumi ya Rahimi ilipokewa kwa shangwe na mashabiki waliokuwa wakipeperusha bendera, lilianza baada ya kusomwa kwa aya za Quran, mcheza soka aliyeonyesha ufundi wake wa kupiga danadana, na wakali wa mapigano ya 'kung-fu' wakionyesha ufundi wao wa Thai Boxing.

"Linalenga kubadili mitazamo ya watu ili kuwaweka mbali na vita na uadui," alisema shabiki wa Rahimi, Attah Mohammad Yousufzai, ambaye ni meneja wa fedha katika kampuni ya mipangombinu ya Kabul.

"Linalenga kuwaonyesha namna ya kupambana huku mnaendelea kupendana."

Rahimi alitwaa mkanda huo kwa ushindi wa TKO uliomaliza pambano ambalo lilikuwa na masumbwi machache yaliyotua vizuri, lililochezwa katika hema ambalo kwa kawaida hutumika kwa mikutano ya kitaifa ya wazee wa kikabila lakini lililopambwa kwa taa kama za jiji la Las Vegas na muziki kutoka katika mitambo ya teknolojia ya kisasa.

"Leo ni mwanzo," Rahimi alisema baada ya pambano hilo, ambalo awali alitamba kumpiga Mtanzania kabla ya raundi ya tatu baada ya Mbelwa kudai kwamba angeshinda kwa KO ya raundi ya nne. "Mkanda huu ni wangu, mkanda huu ni wa Wafghanistan, ni wenu. Nawapenda."