Wednesday, October 31, 2012

MTANZANIA APIGWA TKO PAMBANO LA KUTANGAZA AMANI AFGHANISTAN

Bingwa wa dunia wa taji la Mabara la WBO, Hamid Rahimi akishangilia ushindi baada ya kumpiga Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Bingwa wa dunia wa taji la Mabara la WBO, Hamid Rahimi akishangilia ushindi baada ya kumpiga Said Mbelwa wa Tanzania mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi akimuadhibu Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
Hamid Rahimi (kulia) akizichapa na Said Mbelwa (kushoto) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi (kulia) akizichapa na Said Mbelwa (kushoto) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS

Hamid Rahimi (kushoto) akionyeshana ubabe na Said Mbelwa (kulia) wa Tanzania wakati wa pambano lao mjini Kabul jana jioni. Picha: REUTERS
      

KABUL, Afghanistan
MASHABIKI waliojaa furaha wa mjini Kabul walivamia ulingo kushangilia ushindi katika pambano la kwanza la ngumi za kulipwa nchini Afghanistan, baada ya Hamid Rahimi kumpiga Mtanzania Said Mbelwa katika raundi ya saba.

Bondia wa Afghan, Rahimi alimdunda Mbelwa jana jioni na kutwaa mkanda wa ubingwa wa Mabara wa WBO wa uzito wa kati katika pambano lililopewa jina la "Pigana kwa Ajili ya Amani" katika mji ambao unafahamika zaidi kwa vishindo vya milio ya risasi badala ya masumbwi ya 'uppercuts' na 'jabs'.

Waandaaji wamelenga kutumia pambano hilo, ambalo lilihudhuriwa na mashabiki 1,500 waliolipa kiingilio cha angalau dola 100 (Sh. 156,000) ambazo ni zaidi ya mshahara wa mwezi mzima kwa raia wengi wa Afghan, kwa ajili ya kupromoti michezo kama mbinu ya kuwaunganisha Waafghanistan baada ya miongo kadhaa ya vita.

"Pambano hili litatoa somo kwa Wataliban na vikundi vingine vinavyopingana na serikali kuacha kupambana kwa silaha  na kwamba wanaweza kupambana kusaka uongozi bila ya uhalifu," alisema Mohammad Asif Sahibi (28) wakati akishuhudia pambano hilo.

Pambano la jana, ambalo kila ngumi ya Rahimi ilipokewa kwa shangwe na mashabiki waliokuwa wakipeperusha bendera, lilianza baada ya kusomwa kwa aya za Quran, mcheza soka aliyeonyesha ufundi wake wa kupiga danadana, na wakali wa mapigano ya 'kung-fu' wakionyesha ufundi wao wa Thai Boxing.

"Linalenga kubadili mitazamo ya watu ili kuwaweka mbali na vita na uadui," alisema shabiki wa Rahimi, Attah Mohammad Yousufzai, ambaye ni meneja wa fedha katika kampuni ya mipangombinu ya Kabul.

"Linalenga kuwaonyesha namna ya kupambana huku mnaendelea kupendana."

Rahimi alitwaa mkanda huo kwa ushindi wa TKO uliomaliza pambano ambalo lilikuwa na masumbwi machache yaliyotua vizuri, lililochezwa katika hema ambalo kwa kawaida hutumika kwa mikutano ya kitaifa ya wazee wa kikabila lakini lililopambwa kwa taa kama za jiji la Las Vegas na muziki kutoka katika mitambo ya teknolojia ya kisasa.

"Leo ni mwanzo," Rahimi alisema baada ya pambano hilo, ambalo awali alitamba kumpiga Mtanzania kabla ya raundi ya tatu baada ya Mbelwa kudai kwamba angeshinda kwa KO ya raundi ya nne. "Mkanda huu ni wangu, mkanda huu ni wa Wafghanistan, ni wenu. Nawapenda."

No comments:

Post a Comment