Wednesday, December 26, 2012

YALIYOJIRI KWENYE VODACOM KRISMAS BONANZA

Wanaumeeeee....! Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ‘TMK Wanaume Halisi’ Juma Nature, akiburudisha mamia ya mashabiki waliohudhuria kwenye ‘Vodacom Krismass Bonanza’ katika ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana, Vodacom Tanzania  imedhamini Bonanza hilo katika kipindi hiki cha sikukuu.

Mapanga shyaaa...! Mmoja wa wasanii kutoka kundi la TMK Wanaume Halisi, Rashid Ziada, maarufu ‘KR Mula’ akifanya show mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria kwenye  ‘Vodacom Krismass Bonanza’ katika ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana, Vodacom Tanzania  imedhamini Bonanza hilo katika kipindi hiki cha sikukuu.

Watoto ndani ya bwawa la kuogelea ‘swimming pool’ wakifurahia moja ya michezo waliyoandaliwa Vodacom Tanzania, katika Vodacom Krismass Bonanza lililofanyika kwenye ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana

Hapa ni mwendo tu hadi Zenji....! Mtoto huyu naye hakuwa nyuma katika kufaidi maraha ya kucheza na bata kwenye ‘swimming pool’ wakati akifurahia moja ya michezo waliyoandaliwa Vodacom Tanzania, katika Vodacom Krismass Bonanza lililofanyika kwenye ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana

No comments:

Post a Comment