Wednesday, December 26, 2012

CHICHARITO AIPAISHA MANCHESTER UNITED, MANCHESTER CITY YALIZWA NA SUNDERLAND KUTOKANA NA GOLI LILILOFUNGWA NA STRAIKA WAO WA ZAMANI ALIYEONEKANA KIMEO KWA KOCHA MANCINI -- ADAM JOHNSON… JUAN MATA APIGA BAO PEKEE LILILOIPA CHELSEA RAHA X-MASS…

Gooooooohh....Chezea Chicharito eeenh! Straika Javier Hernandez "Chicharito" wa  Manchester United (kushoto) akifunga goli la ushindi dhidi ya kipa wa  Newcastle United, Tim Krul wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, leo Desemba 26, 2012. (Picha: REUTERS)
Robin van Persie wa Manchester United (kulia) akichuana na James Perch wa Newcastle Unitedwakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, leo Desemba 26, 2012. (Picha: REUTERS)

Wachezaji wa Newcastle United wakishangilia wakati refa Mike Dean akithibitisha kwamba goli la kujifunga la Jonny Evans wa Manchester United ni halali wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, leo Desemba 26, 2012. (Picha: REUTERS)
Dah... nd'o tushaumbuka tena! Straika Carlos Tevez wa Manchester City akionekana kusikitika baada ya timu yake kuchezea kichapo mbele ya Sunderland wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Desemba 26, 2012. (Picha: REUTERS)

Aiya weee... iiiiiiihh...nalia mie..! Sergio Aguero wa Man City akisikitika baada ya baada ya timu yake kuchezea kichapo mbele ya Sunderland wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Desemba 26, 2012. (Picha: REUTERS)
Mancini akiwa hoi baada ya kichapo.
Yaya Toure wa Manchester City (kushoto) akilalamika kwa refa Kevin Friend
Mata akipiga na kuifungia Chelsea dhidi ya Norwich leo Desemba 26, 2012
Mataaaaaaa....!

LONDON, England
MANCHESTER United iliendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya pointi saba leo baada ya kushinda 4-3 dhidi ya Newcastle wakati mahasimu wao Manchester City wanaowafuatia katika nafasi ya pili wakipata kipigo kisichotarajiwa cha bao 1-0 kutoka kwa Sunderland.

Ushindi wa Man U ulitokana na goli la dakika ya mwisho wa mechi lililowekwa wavuni na mshambuliaji Javier Hernandez "Chicharito"  huku mabao mengine yakifungwa na Jonny Evans, Patrice Evra na Robin van Persie.

Man U walilazimika kutoka kuwa nyuma mara tatu 'kuibania' ushindi Newcastle.

Goli lililoimaliza Manchester City lilifungwa na straika wa zamani wa mabingwa hao wa England aliyeonekana hafai kwa kocha wao Roberto Mancini,  Adam Johnson.

Hadi sasa, Man City wako nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nne tu dhidi ya Chelsea ambao walishinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Norwich City, mfungaji akiwa Juan Mata.


MATOKEO YA MECHI ZA LEO ENGLAND
Everton           2 Wigan            1 
Fulham            1 Southampton      1 
Man U             4 Newcastle        3 
Norwich           0 Chelsea          1 
Reading           0 Swansea City     0 
Sunderland        1 Man City         0 

No comments:

Post a Comment