Wednesday, December 26, 2012

PRECISION AIR YAMZAWADIA CHRISTOPHER KATONGO

Katongo (katikati) akikabidhiwa mfano wa tiketi na maafisa wa Precision Air.
Katongo akiwa na baadhi ya memba wenzake wa timu ya taifa ya Zambia na maafisa wa Precision Air.
Katongo (wa pili kushoto) akiwa na maafisa wa Precision Air.
Duh... Tiketi ya ukweli!
Shirika la ndege nchini, Precisionair, limemzawadia mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2012, Christopher Katongo, tiketi ya kwenda na kurudi  kwa watu wawili sehemu yoyote ambapo ndege hiyo inafanya safari zake.

Precision Air ilikabidhi tiketi hiyo jijini Lusaka kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam.

Precision Air pia ilitoa punguzo kwa tiketi za wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia ambao walikuwa walikuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika Desemba 23, 2012.

Katika makabidhiano hayo ambayo yalifanyika kwenye uwanja wa ndege wa jijini Lusaka muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ambayo ilihudhuriwa na balozi wa Zambia nchini Tanzania, Bi. Grace Mujuma, Bi. Chiza alisema Shirika la Precision Air limemzawadia tiketi Katongo kwa kuwa balozi mzuri ndani na nje ya bara la Afrika.

Mchezaji bora wa Afrika ataweza kuzitumia huduma za shirika letu la Precisionair na pia kulitangaza ndani na nje ya bara letu la Afrika.

Shirika hilo la Precision Air linafanya safari zake katika miji ya; Lubumbashi - Kinshasa - Dar na Kinshasa – Harare, Lusaka, Kisangani - Kigali – Entebbe, na Comoro.

Katongo, amenyakua zawadi ya tiketi toka Precision Air wiki kabla ya kutua nchini, baada ya kutangazwa mshindi wa Tuzo hizo za BBC za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2012 huku akiwapiku wachezaji nyota wanaotesa katika ligi za majuu kama Didier Drogba, Yaya Toure, Demba Ba na Younes Belhanda.

No comments:

Post a Comment