Tuesday, December 11, 2012

WACHEZAJI ZANZIBAR HEROES WAFUNGIWA KWA KUGAWANA MKWANJA WA CHALENJI

Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichocheza mechi ya Kombe la Chalenji dhidi ya Burundi katika hatua ya robo fainali
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakimbeba kocha wa Salum Bausi baada ya kutwaa ushindi wa tatu kufuatia kuifunga Tanzania Bara kwa matuta 6-5
Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Haroub Nadir akimzuia mshambuliaji wa trimu ya Zanzibar Heroes, John Boko wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
Mchezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Athuman Chuji akimtoka beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Sabri Alliy Makame wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda jana

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni miongoni mwa wachezaji 16 waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.

Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.


Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Kilimanjaro Stars ta Tanzania Bara kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.


Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.


Hata hivyo, katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama hayo yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu kwamba mara zote walipewa stahili zao.


Kwa upande wake, kocha wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, alisema hatua hiyo ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.
Tayari ZFA Taifa walishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa klabu wanazochezea wachezaji hao.


Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutajwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.


Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda kwenye Chalenji ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (KMkM), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).


Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed (Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam) na washambuliaji, Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).
CHANZO: bongostaz.blogspot.com

---------------------

No comments:

Post a Comment