Tuesday, December 11, 2012

BABA AMCHARANGA MAPANGA NA KUMUUA KINYAMA BINTI YAKE WA MIAKA SABA... YADAIWA ETI KISA NI UGOMVI KATI YAKE NA MKEWE... MTOTO ALIREJEA KWAO AKITOJKEA MADRASA NA KUKUTA UGOMVI MKUBWA WA WAZAZI WAKE... ALIPOPIGA KELELE AKIOMBA BABA ASIMPIGE MAMAYE...AKAUAWA YEYE... NI YOMBO BUZA, TEMEKE DAR!

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Binti anayetajwa kuwa na miaka saba aitwaye Gift Mustafa, ameuawa kinyama kwa kucharangwa mapanga na baba yake Mustafa Mchele, 37, nyumbani kwao Yombo Buza, Temeke jijini Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni ugomvi mkali ulioibuka kati ya baba yake huyo na mama yake aitwaye Zulfa Mathias, 23.

Mauaji hayo ya kinyama yametokea usiku wa kuamkia jana, majira ya saa 1:00 usiku katika eneo la Buza na kusababaisha watu kibao kujaa na kutaka kuchukua sheria mkononi dhidi ya mtuhumiwa, Mustafa Mchele. Polisi waliwahi eneo la tukio na kumuokoa baba huyo asiuawe na wananchi wenye hasira baada ya kurusha risasi kadhaa hewani ili kuwatawanya.

Imedaiwa na baadhi ya mashuhuda kuwa Gift alipigwa mapanga mara kadhaa mwilini ikiwamo kichwani na usoni na ubongo wake ulitawanyika na hivyo akauawa papo hapo.

Inaelezwa kuwa Gift alikuwa amerejea kutoka madrasa na aliposikia baba na mama yake wakigombana, alijaribu kumwita baba yake ili wasiendelee kugombana na ndipo baba yake alipomgeukia yeye na kumcharanga mapanga hadi kumuaa.

Hata hivyo, haikufahamika chanzo hasa cha ugomvi baina ya wazazi hao wa Gift.

Inaelezwa kuwa Mustafa alimjeruhi pia mkewe kwa kumcharanga panga mkononi na usoni.

Englibert Kiondo ambaye ni Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa (Mustafa Mchele) bado anashikiliwa na polisi na mwili wa marehemu uko katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke. Zulfa ambaye ni mama wa marehemu Gift, ameruhusiwa kutoka hospitalini na kwenda kuugulia majeraha nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment