Sunday, December 23, 2012

STURRIDGE KUPIMA AFYA LIVERPOOL LEO


Daniel Sturridge


Daniel Sturridge akiugulia maumivu ya misuli ya nyuma ya paja wakati wa mechi yake ya mwisho kwa Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion kwenye Uwanja wa The Hawthorns mjini West Bromwich, England Novemba 17, 2012.

Daniel Sturridge akiugulia maumivu ya misuli ya nyuma ya paja wakati wa mechi yake ya mwisho kwa Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion kwenye Uwanja wa The Hawthorns mjini West Bromwich, England Novemba 17, 2012.

Daniel Sturridge wa Chelsea akishuhudia shuti lake likipanguliwa na kipa wa West Brom, Boaz Myhill wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya West Bromwich Albion kwenye Uwanja wa The Hawthorns mjini West Bromwich, England Novemba 17, 2012. Katika mechi hiyo ya mwisho kwa Sturridge klabuni Chelsea, timu yake ililala 2-1.

Daniel Sturridge akijiandaa kuanza mpira pamoja na Fernando Torres baada ya kufungwa goli katika mechi yake ya mwisho akiwa na Chelsea dhidi ya West Brom kwenye Uwanja wa The Hawthorns mjini West Bromwich, England Novemba 17, 2012.

Daniel Sturridge wa timu ya taifa ya England akionekana mwenye fadhaa baada ya kufungwa goli wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Sweden kwenye Uwanja wa Friends Arena mjini Stockholm, Sweden Novemba 14, 2012. England ilichapwa 4-2. Ibrahimovic alipiga hat-trick likiwamo goli kali la 'tiktaka' ya umbali wa mita 30.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Daniel Sturridge anatarajiwa kupima afya klabuni Liverpool leo kwa ajili ya uhamisho utakaogharimu paundi milioni 12.

Liverpool wameafikiana dili hilo na Chelsea kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 23 na mkataba wa kumlipa mshahara wa paundi 60,000 kwa wiki.

Hata hivyo, uhamisho wowote hautarajiwi kuthibitishwa hadi Januari wakati dirisa la usajili litakapofunguliwa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City, amecheza mechi saba tu za ligi kuu kwa Chelsea msimu huu na amefunga goli moja.

Mechi yake ya mwisho akiwa na The Blues ilikuwa ni ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa West Bromwich Albion Novemba 17.

Sturridge hajacheza tangu Rafael Benitez alipowasili Stamford Bridge, kutokana na maumivu ya misuli ya nyuma ya paja.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anavutiwa na Sturridge na alijaribu kumsajili kwa mkopo Agosti, lakini mshambuliaji huyo wa Chelsea alitaka uhamisho kamili.

Rodgers amedhamiria kuimarisha safu yake ya ushambuliaji baada ya kumruhusu Andy Carroll ajiunge na West Ham kwa mkopo Agosti na kisha akamkosa mshambuliaji wa zamani wa Fulham, Clint Dempsey katika siku ya mwisho ya usajili.

No comments:

Post a Comment