Saturday, December 22, 2012

REAL MADRID YALALA TENA, HATMA YA MOURINHO SASA SHAKANI

Cristiano Ronaldo (kulia) na Karim Benzema wa Real Madrid wakiwa wamejaa fadhaa baada ya Francisco R. Alarcin Isco wa Malaga kufunga goli la kuongoza wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Real walilala 3-2.
Iker Casillas wa Real Madrid akionekana mnyonge kwenye benchi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Real walilala 3-2.

Iker Casillas wa Real Madrid akionekana kufadhaika
kwenye benchi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Real walilala 3-2.

Iker Casillas wa Real Madrid akijifunika uso kwa fadhaa akiwa benchi baada ya Roque Santa Cruz wa Malaga kuifungia timu yake goli la pili wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Malaga walishinda 3-2.

Iker Casillas wa Real Madrid akionekana kufadhaika
kwenye benchi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Real walilala 3-2.

Iker Casillas wa Real Madrid akionekana kufadhaika
kwenye benchi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga, Hispania leo Desemba 22, 2012. Real walilala 3-2.

REAL  Madrid imeendelea na mwendo mbaya wa msimu baada ya leo kukumbana na kipigo kingine wakati walipofungwa 3-2 dhidi Malaga katika mechi ambayo kocha Jose Mourinho alifanya maamuzi ya kustusha kwa kumtupa benchi nahodha Iker Casillas kwa mara ya kwanza katika miaka 10.

Kipigo kinamaanisha kwamba Real sasa wako pointi 16 nyuma ya vinara Barcelona, ambayo leo ilitoa kipigo cha 16 katika mechi 17 za msimu huu wa La Liga wakati iliposhinda 3-1 ugenini dhidi ya Valladolid huku Lionel Messi akifunga goli lake la 91 mwaka 2012.

Wakati ligi ya Hispania inaenda mapumziko ya wiki mbili kupisha majira ya baridi baada ya mechi za wikiendi hii, kuna maswali kama Mourinho atarejea tena madarakani wakati ligi itakaporejea tena Januari.

Roque Santa Cruz ndiye aliyeamua matokeo ya mechi hiyo, akifunga mara mbili katika kipindi cha pili baada ya kuingia akitokea benchi na kumuongezea presha ya ajira yake Mourinho.

Isco aliwafungia Malaga goli walilostahili la kuongoza dakika nne baada ya mapumziko, lakini piga-nikupige katika lango la wenyeji iliwapa Madrid goli la kusawazisha katika dakika ya 69 kupitia goli la kujifunga la Sergio Sanchez.

Lakini Santa Cruz alibadili mambo kwa wenyeji, akifunga magoli mawili ndani ya dakika tatu kufuatia pasi tamu za Joaquin na kuwafanya Real wawe nyuma 3-1.

Goli la Karim Benzema la dakika ya 82 lililonekana kama la kupunguza machungu tu.

Madrid walio katika nafasi ya tatu wanaonekana kuzidi kupoteza matumaini ya ubingwa huku Malaga walio katika nafasi ya nne wakipanda hadi pointi mbili nyuma yao baada ya ushindi huo.

Mourinho alimshangaza kila mmoja kwa kumtupa benchi nahodha Casillas na kumpa nafasi isiyotegemewa kipa chaguo la pili Antonio Adan na hakuwa na la kufanya kuikoa timu hiyo katika kipigo.
 
 

No comments:

Post a Comment