Thursday, December 13, 2012

SHABIKI WA KUFA NA KUZIKANA

Wachezaji wa Udinese wakishangilia

SHABIKI wa soka nchini Italia alijipatia umaarufu nchini humo kwa kuwa shabiki wa pekee kufika uwanjani wakati wa mechi ya soka ya ligi kuu ya Italia (Serie A) kuunga mkono timu yake.

Arrigo Brovedani -- shabiki wa kilabu ya Udinese -- alijikuta akiwa shabiki peke yake katika uwanja wa Sampdoria wenye maelfu ya viti usiku wa majira ya baridi.

Alizomewa na kukejeliwa na mashabiki wa timu ya wenyeji Sampdoria.

Lakini Arrigo alipeperusha bendera yake na kushangilia timu yake na kisha kuondoka uwanjani mshindi kwani timu yake hatimaye ilishinda mabao 2-0 huku mashabiki hasimu wakiamua kumpongeza kwa kumpeleka eneo la kujivinjari angalau kwa kinywaji.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment