Tuesday, December 4, 2012

SELCOM PAYPOINT YAANZA KUUZA VOCHA ZA ZUKU...!

Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza rasmi Kampuni hiyo kuanza kuuza vocha za kulipia king’amuzi cha Zuku kupitia vituo mbalimbali vya Selcom Paypoint. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania, Fadhil Mwasyeba.

Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori , akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya huduma wanazotoa ikiwa ni pamoja na ulipiaji wa bili mbalimbali kama za simu za makampuni yote, Luku, Startime, tiketi za treni za jijini Dar es Salaam, kulipia ada za mitihani (NECTA), kuangalia matokeo na sasa Zuku.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba  akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba kushoto akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku, wengine ni  Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori   na Meneja wa Bidhaa na uboreshwaji wa viwango Julio Batilia .

Waandishi wa Habari Rehema Kilagwa wa NIPASHE (mbele kulia), Mwasiti wa The Guardian (wa pili kulia) na wengine wakifuatilia maelezo kutoka kwa kina Mgori wa SelCom na Fadhili wa Zuku (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelezea namna wateja wanavyoweza kununua vocha za Zuku kupitia simu za mikononi leo Desemba 4, 2012.

Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba (wa pili kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya kulipia king'amuzi cha Zuku kwa njia ya mtandao na Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori,  makubariano hayo yamefanyika Dar es salaam Leo kwa ajili ya kurahisisha hudumu hio. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka Selcom na Zuku.

No comments:

Post a Comment