Wednesday, December 5, 2012

RONALDO ASAIDIA USHINDI REAL, AFUNGA BAO LAKE LA 61 MWAKA 2012... PSG WAMALIZA VINARA WA KUNDI LAO

Wachezaji wa Man City, kutoka kulia, Sergio Aguero, Carlos Tevez na Pablo Zabaleta wakitoka uwanjani hoi baada ya kukalishwa na Burussia Dortmund
Kostas Mitroglou (wa pili kulia) wa Olympiakos akishangilia bao lake tamu la shuti la mkunjo wa ndizi lililoizamisha Arsenal 2-1 jana usiku.
Cristiano Ronaldo (katikati) wa Real Madrid akishangilia kufunga goli la kuongoza la timu yake pamoja na wachezaji wenzake Karim Benzema (kushoto), CJose Callejon (katikati) na Kaka (kulia) wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdam kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid, Hispania jana Desemba 4, 2012.

CRISTIANO Ronaldo alifunga goli lake la 61 kwa mwaka 2012 wakati Real Madrid ilipoisambaratisha Ajax 4-1 kwenye Uwanja wa Bernabeu.

Mshambuliaji huyo zamani wa Manchester United (27), alifungua akaunti yao ya mabao kufuatia krosi ya Karim Benzema kabla ya Jose Maria Callejon kuongeza la pili.

Kaka kisha akawakumbusha mashabiki enzi wake wakati alipopiga shuti la mkunjo wa ndizi kwa mguu wa kushoto na kuwafungia Real bao la tatu baada ya mpira kugonga nguzo na kutinga wavuni lakini Derk Boerrigter wa Ajax akapunguza moja.

Callejon alikamilisha ushindi baadaye na kukamilisha ushindi mnono wa Real, ambao hata hivyo walimaliza wakiwa wa pili nyuma ya vinara Borussia Dortmund katika Kundi D.

Ronaldo sasa amefunga magoli 167 katika mechi 165 kwa Real tangu ajiunge nao mwaka 2009, lakini mafanikio yake ya mwaka 2012 yamefunikwa vibaya na nyota wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye anaweza kuifikia rekodi ya Gerd Mueller ya muda wote ya kufunga magoli 85 katika mwaka mmoja wa kalenda kama atafunga goli moja leo usiku dhidi ya Benfica katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kwingineko, Paris Saint-Germain walimaliza wakiwa vinara wa kundi A baada ya Ezequiel Lavezzi kutumia makosa ya ya kipa na kuwapa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Porto.

Thiago Silva alifunga kwa kichwa goli la kuongoza la PSG kabla ya Jackson Martinez kuwasazishia Porto, lakini Lavezzi akaiweka kileleni mwa kundi timu hiyo ya kocha Carlo Ancelotti wakati shuti lake dhaifu lilipomponyoka kipa wa Porto, Helton. Porto walikuwa tayari wamefuzu na wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili.

Katika mechi ambayo ilicheleweshwa kwa muda kutokana na barafu, Dinamo Zagreb walipata ushindi wao wa kwanza na pointi pekee ya Kundi A wakati Ivan Krstanovic alipofunga penalti ya dakika za majeruhi na kuambulia sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Dynamo Kiev.

Katika Kundi C, goli kutoka kwa Danny liliwapa Zenit St Petersburg ushindi usiotarajiwa wa 1-0 dhidi ya washindi wa pili AC Milan kwenye Uwanja wa San Siro, ushindi uliowapa nafasi ya kucheza Ligi ya Europa.

Manchester City ilimaliza vibaya kampeni zao kwa kukosa hata nafasi ya kucheza Ligi ya Europa baada ya jana kufungwa tena bao 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund. Klabu hiyo tajiri imetolewa kwa aibu katika hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuambulia pointi tatu tu ambazo zimetokana na sare tatu na vipigo vitatu katika Kundi D lililoshuhudia Dortmund na Real zikisonga mbele huku Ajax ikimaliza katika nafasi ya kucheza Ligi ya Europa.

Arsenal licha ya kuwa tayari ilishafuzu na kuweka rekodi ya kufuzu kwa hatua ya 16-Bora kwa misimu 13 mfululizo, iliendelea na mwanzo wake mbaya wa msimu kwa kuchapwa 2-1 ugenini dhidi ya Olympiakos mjini Athens.  

Mwendo mbovu wa Arsenal uliwanyima fursa ya kumaliza vinara wa Kundi B baada ya vinara Schalke kushikiliwa katika sare ya 1-1 ugenini Ufaransa dhidi ya Montepellier. Schalke wamemaliza wakiwa na pointi 12 wakati Arsenal wamemaliza na pointi 10.

Kikosi cha Arsenal kilichofanya mabadiliko ya wachezaji saba huku Theo Walcott akiwa amepumzishwa na hata hakusafiri na timu, kilianza vyema na Tomas Rosicky akawafungia goli la kuongoza muda mfupi kabla ya mapumziko.

Lakini Olympiakos walisawazisha kwa shuti la jirani na lango la Giannis Maniatis na wakapata ushindi waliostahili kupitia kwa shuti zuri la upinde kutoka kwa Kostas Mitroglou.

Arsenal walikuwa tayari wameshafuzu kwa hatua ya 16 lakini wamemaliza wakiwa wa pili.

Jambo hilo linamaanisha sasa wataangukia mikononi mwa timu kama Barcelona, Paris Saint-Germain au Borussia Dortmund katika hatua ya 16-Bora. 


Timu zilizofuzu kwa hatua ya 16-Bora Ulaya:

Kundi A: PSG, Porto
Kundi B: Schalke, Arsenal
Kundi C: Malaga, AC Milan
Kundi D: Dortmund, Real Madrid
Kundi E: Shakhtar Donetsk
Kundi F: Bayern Munich, Valencia
Kundi G: Barcelona
Kundi H: Manchester United

MATOKEO YA JANA USIKU UEFA
  • Borussia Dortmund 1 - 0 Man City 
  • Olympiakos 2 - 1 Arsenal 
  • AC Milan 0 - 1 Zenit St P'sbg 
  • Din Zagreb 1 - 1 Dynamo Kiev
  • Malaga 2 - 2 Anderlecht 
  • Montpellier 1 - 1 Schalke 04 
  • Real Madrid 4 - 1 Ajax
     
    RATIBA YA MECHI ZA LEO USIKU UEFA



    MISIMAMO YA MAKUNDI UEFA

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Points

    1. Paris SG 6 11 15
    2. FC Porto 6 6 13
    3. Dynamo Kiev 6 -4 5

    Din Zagreb 6 -13 1

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Schalke 04 6 4 12
    2. Arsenal 6 2 10
    3. Olympiakos 6 0 9
    4. Montpellier 6 -6 2

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Malaga 6 7 12
    2. AC Milan 6 1 8
    3. Zenit St P'sbg 6 -3 7
    4. Anderlecht 6 -5 5

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Borussia Dortmund 6 6 14
    2. Real Madrid 6 6 11
    3. Ajax 6 -8 4
    4. Man City 6 -4 3

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Shakhtar Donetsk 5 5 10
    2. Juventus 5 7 9
    3. Chelsea 5 1 7
    4. Nordsjaelland 5 -13 1

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Bayern Munich 5 5 10
    2. Valencia 5 6 10
    3. BATE Borisov 5 -3 6
    4. Lille 5 -8 3

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Barcelona 5 6 12
    2. Benfica 5 0 7
    3. Celtic 5 0 7
    4. Spartak Moscow 5 -6 3

    Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
    1. Man Utd 5 4 12
    2. Galatasaray 5 0 7
    3. CFR Cluj-Napoca 5 1 7
    4. Braga 5 -5 3

No comments:

Post a Comment