Sunday, December 9, 2012

RVP AIZAMISHA MAN CITY USIKUUU... CHEZEA RVP WEWE?

Wayne Rooney (katikati) akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Man City pamoja na wachezaji wenzake wa Man Utd, Ashley Young (kushoto) na Robin van Persie wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad leo
Yaya Toure (kulia) akishangilia goli lake

MANCHESTER, England
GOLI kali la ‘fri-kiki’ kutoka kwa Robin van Persie katika dakika za majeruhi liliwapa Manchester United ushindi wa ugenini wa 3-2 dhidi ya mabingwa Manchester City leo na hivyo kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya pointi sita.


Licha ya Man City kuonekana wakitawala mechi, Wayne Rooney aliwafungia wageni goli la utangulizi kinyume na mwelekeo wa mchezo katika dakika ya 16 kutokana na shuti ‘jepesi’ la chini lililozama pembeni, ndani ya nyavu ndogo kabla mshambuliaji huyo hajafunga goli lake la pili kwenye mechi hiyo katika dakika ya 29.


Man City walifunga goli lao la kwanza kupitia kwa Yaya Toure katika dakika ya 60 kabla hawajasawazisha katika dakika ya 86 kutokana na shuti “tamu” la Pablo Zabaleta, lakini hisia zozote za sare zilizimwa muda mfupi baadaye wakati Van Persie alipoiga ‘fri-kiki’ kali iliyoguswa na Samir Nasri kabla ya kujaa wavuni.


Shangwe za Man U zilikatizwa wakati beki wao Rio Ferdinand alipojeruhiwa na kujikuta akivuja damu juu ya jicho lake la kushoto baada ya kupigwa na na kitu kilichorushwa na mashabiki.


Matokeo hayo yalihitimisha takriban rekodi ya miaka miwili ya kutofungwa nyumbani kwa Man City katika Ligi Kuu ya England huku Man U ikiendelea kutesa kileleni kwa kuwa na pointi 39 kutokana na mechi 16, wakati Man City wakibaki katika nafasi ya pili huku wakiwa na pointi 33.
-------

No comments:

Post a Comment