Wednesday, December 26, 2012

RONALDO AKOSA 'TUZO' HATA YA MCHEZAJI BORA WA REAL MADRID 2012, MASHABIKI WAMCHAGUA CASILLAS NA RAMOS... RONALDO AWA WA TATU


WAKATI Cristiano Ronaldo akisubiri kujua kama ataweza kumpiku Lionel Messi katika kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2012, mashabiki wa klabu yake ya Real Madrid hawaoni kama Mreno huyo anastahili hata kuwa mwanasoka bora wa klabu hiyo.

Kipa Iker Casillas na Sergio Ramos ndiyo wanasoka bora wa Real Madrid kwa mwaka 2012, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa mashabiki 30,000 wa klabu hiyo.


Mashabiki wamewapa wastani wa 6.9 wachezaji hao wawili, huku Cristiano Ronaldo akiangukia nafasi ya tatu akipata wastani wa 6.6 ya ubora. Xabi Alonso, Callejon, Ozil na Benzema ni wachezaji wengine wanne wa Madrid ambao wastani waliopata unazidi 6, huku Pepe naye akikaribia.


Kulikuwa na orodha ndefu ya wachezaji waliopata wastani wa chini ya 5, (Arbeloa, Coentrao, Di MarĂ­a, Essien, Modric, Kaka, Adan, Albiol, Carvalho na Nacho) pamoja na kocha Jose Mourinho, ambaye mashabiki wamempa wastani wa 3.5.


Khedira, Marcelo, Varane, Higuain na Morata wameuvuka kidogo wastani wa kucheza kwa kiwango cha ubora, wakati wastani wa ubora kwa kikosi kizima ulikuwa ni 5.1.

No comments:

Post a Comment