Wednesday, December 26, 2012

MESSI AMPELEKA MWANAE KWA MARA YA KWANZA KWAO ARGENTINA

Messi akimbusu mwanae Thiago huku akifuatwa na mchumba wake Antonella wakati wakiwasili nchini kwao Argentina

LIONEL Messi hivi sasa yuko mapumziko nyumbani kwao Rosario, Argentina. Aliwasili asubuhi ya Jumatatu na atakaa huko hadi Januari 2 wakati atakaporejea mazoezini Barcelona.

Mshambuliaji huyo ameambatana na mchumba wake Antonella na mwanae mwenye umri wa wiki nane, Thiago, ambaye ametembelea nchi ya baba yake kwa mara ya kwanza.

"Niko Rosario sasa na familia yangu nzima. Wazazi wangu walikuja kunipokea uwanja wa ndege. Kuna joto sana katika mji wa nyumbani kwetu, lakini nina furaha nimerejea nyumbani", alisema nyota huyo wa Barca kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘Weibo’.

"Nimemaliza vyema kwa magoli na rekodi, lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama tungebeba mataji. Daima nimekuwa nikisema kwamba kilicho muhimu zaidi ni tuzo ya pamoja. Magoli yangu bila ya makombe, haina maana.

"Kuzaliwa kwa Thiago kulikuwa ni jambo kubwa sana kati ya yote yaliyowahi kutokea maishani mwangu. Ilikuwa ni kipindi 'spesho' sana maishani mwangu," supastaa huyo wa Barca alisema katika gazeti la Catalunya la 'El Mundo Deportivo'.

No comments:

Post a Comment