Saturday, December 22, 2012

ARSENAL, MAN CITY, LIVERPOOL ZANG'AA ENGLAND

Luis Suarez wa Liverpool akishangilia baada ya kufunga goli la nne la timu yake wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Fulham kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, England leo Desemba 22, 2012. Liverpool iliua 4-0.
Mikel Arteta wa Arsenal akifunga penalti wakati wa kati ya mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Wigan Athletic kwenye Uwanja wa DW mjini Wigan, England leo Desemba 22, 2012. Arsenal ilishinda 1-0.

Mikel Arteta wa Arsenal akishangilia baada ya kufunga penalti dhidi ya Wigan leo.

ARSENAL, Manchester City na Arsenal zote zimeshinda katika mechi zao za leo za Ligi Kuu ya England.

Penalti ya Mikel Arteta, iliwapa Arsenal ushindi wa tatu mfululizo wakati waliposhinda kwa goli 1-0 dhidi Wigan.

Gareth Barry alifunga goli la dakika ya 92 wakati Manchester City ilipoilaza Reading 1-0 na kupunguza pengo la pointi kileleni mwa msimamo na kufikia pointi tatu nyuma ya vinara Manchester United.

Winga Stewart Downing ambaye ameambiwa kwamba anaweza kuondoka klabuni Liverpool, alicheza kwa kiwango cha juu na kuisaidia timu yake kupata ushindi mnono dhidi ya Fulham na kukwea hadi katika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu.

Martin Skrtel aliumiliki vyema mpira wa kona ya Steven Gerrard na kufumua shuti kali lililotinga wavuni na kuipatia Liverpool goli la kuongoza mbele ya mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield.

Kisha Downing (28) akampikia Gerrard goli la pili kabla ya winga huyo Muingereza kufunga goli lake la kwanza la ligi akiwa na klabu hiyo baada ya kuingia ndani vyema na kufumua shuti lililoenda wavuni.

Luis Suarez alikamilisha ushindi mnono kwa goli la nne akifunga kwa kutumia pembeni ya kiatu.


Matokeo kamili:
No comments:

Post a Comment