Sunday, December 9, 2012

RAIS KIKWETE AJIVUNIA AMANI, UTULIVU WAKATI TAIFA LIKISHEREHEKEA MIAKA 51 YA UHURU TANZANIA BARA

Rais wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili wka gari maalum la jeshi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Mko ngangari? Rais Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.

Kweli mko fiti... nawakubali! Rais Kikwete akiendelea kukagua gwaride wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
     
 
Midundo ya kijeshi-jeshi! "Brass Band" ikiendelea kufanya vitu vyake jukwaani wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
     

Mzee Ruksa, Kabila, Guebuza... wote walikuwepo! Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya uhuru kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Sesemba 9, 2012. Kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, "Mzee Ruksa" Ali Hassan Mwinyi.


Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika).
        
Karibu Mheshimiwa...! Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik akimkaribisha kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo Desemba 9, 2012.
        
Karibu mama...! Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimkaribisha Mama Maria Nyerere kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo Desemba 9, 2012.
     
Karibu bosi..! Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (katikati) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo Desemba 9, 2012.
Shikamoo Mzee Ruksa..! Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimkaribisha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi "Mzee Ruksa" baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo Desemba 9, 2012.
            
 Tuko fiti kuzima fyokofyoko zozote zile...! Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama walioshiriki gwaride mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo Desemba 9, 2012.
Assalam Alleykum mama...! Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume baada ya kuwasili uwanjani wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete na wageni wake wakishuhudia gwaride la askari wa vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
              

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akishuhudia gwaride pamoja na viongozi wengine mbalimbali pamoja na wageni waalikwa. Wanaomfuatia ni Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, Rais wa Namibia, Ifikepunye Pohamba na mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete; kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
  
Vijana wa chipukizi nao waliwepo wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzani Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
Chipukizi wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa na silaha wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzani Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
       
 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbele ya Rais Kikwete wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.
      

Hili ni kundi jingine la askari wa JWTZ. Hapa wakipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikewete wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2012.    
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa anajivunia hali ya amani na utulivu nchini na kuwataka Watanzania waendelee kuienzi hali hiyo.

Rais Kikwete aliyasema hayo mbele ya wageni wake wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Kama ilivyotarajiwa, sherehe hizo zilifana mno kutokana na 'manjonjo' ya askari wa vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama wa taifa waliokuwa wakipita mbele ya amiri jeshi mkuu, Rais Kikwete; ambaye pia alikagua gwaride lao.

Si jambo la kawaida kwa rais kupata nafasi ya kuhutubia wakati wa sherehe za uhuru kama leo. Hata hivyo, Rais Kikwete alitoa maneno machache wakati akiwakaribisha wageni wake mbalimbali, wakiwamo marais kadhaa wa Afrika waliohudhuria sherehe hizo; baadhi yao wakiwa ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, Rais wa Namibia Ikepefunye Pohamba na Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ni miongoni pia watu mashuhuru waliohudhuria sherehe hizo.     


No comments:

Post a Comment