Monday, December 10, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWATUNUKU NISHANI KWA WATUMISHI KWA MWAKA 2012


 Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la 1, Dkt. Mohamed Seif Khatib- Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hito wakati wakisubiri kutunukiwa.
 Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Alhaj Ramadhan Mussa Kijjah-Wizara Fedha, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam. 
  Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Ludovick Silemwa Lemnge Utouh- Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (ii), Ruth Rashid- Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Sanaa na Michezo, Bi Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude)-BASADA, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
 Bi Kidude, akiwa katika pozi baada ya kuvishwa Nishani yake na Rais Kikwete, huku akiimba wimbo wake wa Laiti, kwa poooozi.
 Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Sanaa na Michezo, Muhidin Mwalimu Gurumo-Habari,Utamaduni na Michezo, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Utunzaji Mazingira daraja la (I) Bw. Reginald Abraham Mengi_Kamati ya Nishani, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
 Bw. Mengi akifurahia Nishani yake na kupozi kwa picha na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kutunukiwa.
 Rais Jakaya Kikwete, akimvisha Nishani ya Ushupavu, P.8183 Maj M.A Hassan-Mkoa wa Kigoma, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza mwanamuziki wa Msondo, Muhidin Gurumo, kwa kutunukiwa Nishani ya sanaa na Rais Kikwete.
 Rais Jakaya, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein na mkewe, Bi Mwanamwema, wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha sanaa cha Taifa cha Rwanda wakati wa hafla ya usiku ya miaka 51 ya Uhuru, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Inspekta General, Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar jana usiku.

No comments:

Post a Comment