Sunday, December 2, 2012

RADAMEL FALCAO ASHINDWA KUFURUKUTA WAKATI ATLETICO MADRID IKIPELEKWA MCHAKAMCHAKA NA KUCHAPWA 2-0 NA MAHASIMU WAO REAL MADRID... CRISTIANO RONALDO ATUPIA MOJA, LIONEL MESSI APIGA 2 KUIPA BARCELONA USHINDI WA 5-1 DHIDI YA ATHLETIC BILBAO... CHELSEA YALAMBWA 3-1 NA WEST HAM, BAYERN MUNICH YASHIKILIWA SARE YA 1-1 NA MAHASIMU WAO BORUSSIA DORTMUND... PSG YA KINA ZLATAN IBRAHIMOVIC NAYO YACHAPWA LIGUE 1....MAN U YAJICHIMBIA KILELENI IKIUA 4-3... ARSENAL 'KIMEO' YAPIGWA 2-0 NA SWANSEA

Unatisha...! Cristiano Ronaldo (kulia) akimpongeza mchezaji mwenzake Mesut Ozil wa Real Madrid baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Atletico Madrid wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu leo Desemba 1, 2012. 
Alvaro Arbeloa wa Real Madrid akiosha mpira kwa kichwa wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu leo Desemba 1, 2012.

Ozil (kushoto) akidhibitiwa na beki wa Atletico Madrid 

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishangilia baada ya kutupia goli la kwanza la timu yake dhidi ya Atletico Madrid leo Desemba 1, 2012.
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Uwanja wa Nou Camp leo Desemba 1, 2012. 
Tumekwisha...! Fernando Torres na Juan Mata wa Chelsea wakionekana kama wasioamini kile kinachotokea baada ya kupigwa goli 3-1 na West Ham United katika mechi ya Ligi Kuu ya England leo Desemab 1, 2012.

Lukas Bendtner (katikati) akishangilia goli na wachezaji wenzake wa Juventus wakati wa mechi yao ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia dhidi ya Torino leo Desemba 1, 2012.
Marchisio wa Juventus akishangilia goli alilofunga dhidi ya Torino. Juve ilishinda 3-0.

Wachezaji wa Nice wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya PSG ya kina Zlatan Ibrahimovic wakati wa mechi yao ya Ligue 1, Ligi Kuu ya Ufaransa leo Desemba 1, 2012. Nice ilishinda 2-1.

Goooooh....! Msenegali Mohamed Diame wa West Ham United (kushoto) akishangilia goli alilofunga dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Desemba 1, 2012. 
Lionel Messi wa Barceolona (kulia) akiwafungisha tela mabeki wa Athletic Bilbao wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Camp Nou leo Desemba 1, 2012.
Chicharito na Anderson wa Manchester United wakishagilia goli walilofunga katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading leo Desemba 1, 2012.
MATOKEO MECHI ZA LEO ENGLAND (DESEMBA 1, 2012)
  West Ham      3 - 1 Chelsea
    Arsenal        0 - 2 Swansea
    Fulham        0 - 3 Tottenham
    Liverpool    1 - 0 Southampton
    Man City     1 - 1 Everton
    QPR            1 - 1 Aston Villa
    West Brom  0 - 1 Stoke
    Reading       3 - 4 Man Utd

MATOKEO MECHI ZA LEO LA LIGA, LIGI KUU YA HISPANIA (DESEMBA 1, 2012)
Getafe                  1-0     Málaga    
Valencia               2-5     Real Sociedad    
Barcelona             5-1     Athletic Bilbao    
Real Madrid         2-0     Atlético Madrid


MATOKEO MECHI ZA LEO SERIE A, LIGI KUU YA ITALIA (DESEMBA 1, 2012)
Juventus                  3-0     Torino    


MATOKEO MECHI ZA LEO BUNDESLIGA, LIGI KUU YA UJERUMANI (DESEMBA 1, 2012)
Bayer Leverkusen           1-0     Nurnberg    
FC Augsburg                    1-1     SC Freiburg    
Mainz                               2-1     Hannover 96    
Schalke 04                        1-1     Borussia Monchengladbach    
SpVgg Greuther Fürth      0-1     VfB Stuttgart    
Bayern Munich                1-1     Borussia Dortmun   


MATOKEO MECHI ZA LEO LIGUE 1, LIGI KUU YA UFARANSA (DESEMBA 1, 2012)
Lyon                 1-0     Montpellier    
Bordeaux          2-2     Sochaux    
Gaillard             1-1     AS Nancy
Lille                   0-0     Bastia    
Nice                   2-1     Paris Saint-Germain
Valenciennes     1-0     Stade de Reims

No comments:

Post a Comment