Beckham akiwa na wanae kutoka kushoto Romeo, Cruz na Brooklyn |
Mashabiki wakibeba bango la Beckham ambaye huvaa jezi Na.23 wakati wa mechi yake ya mwisho jana |
Bend it like Beckham (ikunje kama Beckham)... kama unaweza lakini |
Becks akiwajibika katika mechi yake ya mwisho |
Becks akifurahi baada ya kushinda katika mechi yake ya mwisho kuichezea L.A. Galaxy |
Ni raha tuuu.... full kumwagiwa shampeni |
Cruz Beckham akibeba kombe hilo jana |
DAVID Beckham alihitimisha kipindi chake cha miaka mitano na nusu cha kucheza soka Marekani kwa kuisaidia timu yake ya LA Galaxy kutetea Kombe la 'Ligi' la MLS kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Houston Dynamo katika mechi yake ya mwisho kuichezea klabu hiyo.
Houston waliongoza wakati wa mapumziko kupitia shuti kali la Calen Carr, lakini goli la kichwa la Omar Gonzalez na penalti ya utulivu ya Landon Donovan vilibadilisha mwelekeo wa mechi.
Penalti ya pili, iliyofungwa na Robbie Keane katika dakika za majeruhi, ilikamilisha ushindi katika mechi hiyo ilichochezwa mjini Los Angeles.
Beckham (37) kisha akapumzishwa na kushangiliwa na mashabiki ambao waliinuka kumuaga.
"Nina machungu kwa sababu leo ndiyo mwisho," alisema Beckham.
"hapa ni mahala 'spesho' kwangu na pataendelea kuwa hivyo. Nina furaha sehemu ya klabu hii kwa miaka sita na nina furaha imekuwa timu ya mafanikio katika miaka minne iliyopita.
"Naweza nisicheze tena hapa lakini nitaendelea kujitoa katika kusaidia kukua kwa klabu hii, ligi hii na mchezo huu."
Beckham amehusishwa na mipango ya kujiunga na klabu ya Paris St Germain na Monaco, lakini amesisitiza kwamba "hajui" atacheza wapi msimu ujao.
Ni mara ya pili kwa Beckham kubeba Kombe la 'Ligi" la MLS, LA Galaxy ikiwafunga wapinzani wao hao hao 1-0 katika fainali ya mwaka jana.
No comments:
Post a Comment