Thursday, December 13, 2012

POLISI WASTUKIA MPANGO WA KUMUUA JUSTIN BIEBER

Justin Bieber
Tanner Ruane (kushoto) na Mark Staake wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kupanga kumuua Justin Bieber. Mark Staake, ambaye alikuwa amemaliza kifungo na kutoka gerezani, alipewa 'dili' hilo na mfungwa wa ubakaji na mauaji Dana Martin wakati wakiwa pamoja gerezani kwamba akitoka akamuue Bieber. Mark alipotoka akamtafuta binamu yake Tanner ili amsaidie katika mauaji hayo. 
Justin Bieber akiwa na mama yake Pattie Malette.
Justin Bieber akiwa na mama yake Pattie Malette wakati wa tamasha la 40th la kila mwaka tuzo za American Music Awards kwenye Ukumbi wa Nokia Theatre mjini Los Angeles, California Novemba 18, 2012.

WAPELELEZI wamestukia mpango wa mfungwa wa mauaji wa kutaka kumuua na kukata maungo nyeti ya muimbaji kijana Justin Bieber, mtandao wa habari wa KRQE news umeripoti.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Dana Martin -- ambaye hivi sasa anatumikia vifungo viwili vya maisha mjini New Mexico kwa kumbaka na kumuua binti wa umri wa miaka 15 huko Vermont miaka 12 iliyopita -- alimkodi mfungwa mwenzake katika gereza la Las Cruces amsaidie kufanya mfululizo wa mauaji, mojawapo yakiwa mauaji ya muimbaji wa "Beauty and the Beat".

Maafisa wa polisi wamesema mfungwa aliyoachiwa kutoka gerezani hivi karibuni Mark Staake na binamu yake Tanner Ruane walikuwa wamuue nyota huyo wa pop wakati wa onyesho lake ambalo limeuza tiketi zote kwenye ukumbi wa Madison Square Garden mjini New York City mwezi Novemba. Mpango ulikuwa kumnyonga nyota huyo mtoto pamoja na mabodigadi wake kwa kutumia tai, na kisha kuwakata maungo yao ya uzazi.

Kabla ya tukio hilo la kinyama kufanywa, Staake alikamatwa mjini Vermont. Hata hivyo, Martin -- ambaye mtandao wa KRQE umesema ni mtu "anayempenda kupindukia" Bieber na amejichora tattoo ya muimbaji huyo kwenye mguu wake -- aliharibu mpango mwenyewe na kuwasimulia polisi kila walichopanga. Wapelelezi baadaye walirekodi simu baina ya Martin na Ruane ambazo wawili hao walikuwa wakijadilia mauaji hayo.

Ruane anashikiliwa na polisi wa New York, ambao walikuta zana zote zilizopangwa kutumika katika mauaji hayo wakati akikamatwa.

Meneja wa Bieber, Scooter Braun, alizungumza na gazeti la Us Weekly kuhusu mpango huo wa shambulizi, akisisitiza kwamba usalama wa muimbaji huyo ni jambo linalopewa umuhimu wa kwanza na timu yake.

"Tunachukua kila tahadhari kumlinda na kuhakikisha usalama wa Justin na mashabiki wake," Braun aliliambia gazeti la Us.

No comments:

Post a Comment