Saturday, December 29, 2012

NUKUU KALI ZA SOKA ZA MWAKA 2012.... ‘TAKWIMU NI KAMA SKETI-KIMINI, HAZIANIKI KILA KITU HADHARANI'’

Kutoka kwa Zlatan alichosema kuhusu Super Mario na Sepp kuhusu ‘housewives’ hadi kila mmoja alichosema kuhusu Leo Messi, hizi hapa ni baadhi ya nukuu kali za soka katika miezi 12 iliyopita.
USIVAMIE KAZI ZA WATU

"'Kojak' hajawahi kunipigia simu. Jambo hili linanifaya nicheke. Jamaa wale kawaida yao wanakurupuka tu kutoka vitandani. Walimuuza [Thiago Silva kwa PSG] kwa euro milioni 45 na sasa wanataka kumuiba mmoja wetu... Kama wataleta ofa ya euro milioni 25 au euro milioni 30 hapo sawa, lakini kwa nilivyosukumwa niamini, walikuja na euro milioni au 6. [Galliani anapaswa] aende kucheza filamu na sio kutusumbua."

- Mmiliki wa Montpellier, Louis Nicollin alionyesha kutofurahishwa na mipango ya AC Milan ya kutaka kumsajili Mapou Yanga-Mbiwa, hivyo akamfananisha rais wa klabu hiyo Adriano Galliani na muigizaji wa filamu ya kihalifu ya miaka ya 1970 aliyeitwa Kojak, ambaye alikuwa akinyoa upara.

----------------------------------------------------------------------------------------------
 
"Pele alisema kupiga penalti kama nilivyofanya mimi, unapaswa kuwa ‘genius’ ama una wazimu. Mimi najichukulia nina wazimu."

- 2012 ulishuhudia wachezaji kadhaa wakifunga penalti kwa kuidokoa kwa mtindo wa Panenka-style, na jamaa huyo mwenyewe, Antonin Panenka, alikuwa na furaha alipoulizwa kuhusu staili yake hiyo ya upigaji penalti.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Nampenda Balotelli: Yeye ni kichaa zaidi yangu. Anaweza kufunga goli la ushindi halafu akachoma moto hoteli."

- Zlatan akielezea mambo ambayo anaweza kuyafanya Zlatan pekee.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Wanahitaji pesa kumnunua (beki wa kushoto Federico) Balzaretti ... Milan hawawezi hata kununua mkate wa mayai asubuhi, sasa watamnunua nani?"

- Rais wa Palermo, Maurizio Zamparini akiwakumbusha AC Milan kuhusu uwezo wako wa kifedha hivi sasa.
 
MAN TO MAN

"Twende nje tukaongee kiutu-uzima."

- Ni haki kusema kwamba kocha wa timu ya taifa ya Ukraine, Oleg Blokhin hakuwa katika ‘mudi’ ya kujibu mwelekeo wa maswali ya mwandishi mmoja baada ya timu yake kulala dhidi ya England kwenye Euro 2012.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Angeweza kuuawa!"

- Sir Alex Ferguson hakufurahishwa na maamuzi ‘yasiyo ya kiungwana’ ya Ashley Williams kuamua kubutua uliomlenga kisogoni Robin van Persie wakati akiwa ameanguka jirani yake.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Katika miaka mitano ya soka la India, sijawahi kuliona kombe la Ligi Kuu ya soka ya India (I-League) hata mara moja … kama washindi hawajui hata kombe likoje, mnafanya nini (katika ligi hiyo)?"

- Mmiliki wa klabu ya soka ya Pune FC, Rajeev Piramal bado anajiuliza wanacheza kwa ajili ya nini.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Watu wanazungumza s*** kuhusu sisi kama vile sisi ni s*** na makocha wanalazimika kuondoka, lakini huo ni upuuzi."

- Mchezaji wa Reading, Jimmy Kebe akiwakumbusha kila mtu klabuni hapo kwamba bado anaaminika.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Montpellier, mabingwa wa Ufaransa? Kama ningekuwa ni mtu wa klabu Marseille, Paris, Lyon, Lille au Rennes,ningejichoma na soseji kwenye makalio yangu! Ni aibu kiasi gani kwao."

- Mmiliki wa klabu ya Montpellier, Louis Nicollin akielezea namna alivyoshangazwa na timu yake kuzipuku timu kubwa za Ligue 1 na kutwaa ubingwa wa Ufaransa msimu wa 2011-12.

----------------------------------------------------------------------------------------------
 
"Kama Pele anadhani yeye ni Beethoven wa soka basi mimi ni Ronnie Wood, Keith Richards na Bono wa soka, kwa sababu nina hisia kali zaidi (ya soka)."

- Diego Maradona akiendelea na vita yake ya maneno kuhusu nani ni mwanasoka bora wa muda wote.

HIYO NI KAZI YANGU

"Ninapofunga, sishangilii kwa sababu hiyo ni kazi yangu. Mfanyakazi wa posta anapowasilisha barua kwa muhusika anashangilia?"

- Mario akijibu kwa majibu yake yanayotarajiwa wakati alipoulizwa kwanini haonyeshi furaha kama inavyotarajiwa anapofunga magoli.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Hisia hazijajumuishwa katika majukumu yangu ya kazi."

- Kocha wa klabu ya Philadelphia Union, Peter Nowak alitetea maamuzi yake ya kumtema Sebastien Le Toux, kinara wa mabao wa muda wote wa klabu hiyo na kipenzi Na.1 cha mashabiki. Nowak alitimuliwa kazi katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Marekani (MLS), na Le Toux akarejewhwa kikosini wiki kadhaa zilizopita.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Mimi napingana na ‘anti-footballers’ ambao wanadhani kusoma vitabu vingi ama kuwa na utamaduni fulani ndiyo kuwa mjanja. Nazungumza Kifaransa, Kihispania, Kiingereza na nimeanza kujifunza Kichina. Scapin's Deceit, Pythagoras' theorem na 50 Shades of Grey, havina mpango kwangu."

- Nicolas Anelka akipepea bendera ya wanasoka dhidi ya wasomi.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Wiki hii, nimeona kwamba Gary ni mmoja wa wawekezaji katika ujenzi wa hoteli mpya ya mjini Manchester. Jambo hilo linainufaisha vipi timu ya taifa ya England (akiwa kama kocha msaidizi) na Roy Hodgson?"

- Carlos Tevez akipendekeza Gary Neville aweke nguvu katika kazi moja kwa wakati husika.
 
MESSI “MDUCHU” ANA LIGI YA PEKE YAKE

"Messi ni mchezaji bora duniani na utadhani anatokea katika sayari nyingine … Ni vigumu kutafuta neon jingine la kumuelezea Lionel. Huwezi kujua kama ndiyo tayari amefikia kiwango chake cha juu kabisa ama ndiyo kwanza anaelekea kileleni, kwa sababu yuko katika ligi yap eke yake."

- Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabella alishindwa kupata maneno ya kumuelezea nahodha wake kufuatia mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka 2012 mshambuliaji huyo wa Barcelona.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Tunazungumzia magoli 88 kama vile ni kitu cha kawaida – Alichofanya ni balaa. Messi ni kama ana nguvu ya miujiza."

- Mchezaji mwenzake wa timu ya taifa Javier Mascherano alipata maneno machache ya kumuelezea, hata hivyo, kabla Messi hajamaliza mwaka kwa kufunga magoli 91.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Hongera kwa Messi. Anatisha. Anachokifanya ni unashindwa kuamini."

- Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Mchezaji kwa kawaida huonyesha ubora wake wa juu kabisa awapo na miaka kati ya 25 na 29, hivyo sidhani kama nimeshaonyesha ubora wangu wote. Hatuwezi sote kuwa Lionel Messi, hata kama tunataka."
- Winga wa Ajax, Ryan Babel alisema wakati akizungumzia maisha yake ya kukatisha tama klabuni Liverpool.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Itakuwa ni kura ya huruma tu kama utampigia kura mchezaji mwingine. Hamna namna yoyote kwamba Messi hatashinda tuzo hii."

- Kocha wa timu ya taifa ya Korea Kusini, Choi Kang-Hee akisema ya moyoni wakati akieleza ni nani atakayempigia kura ya mshindi wa tuzo ya Ballon' d’Or wakati sanduku la kura litakapofika kwake.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Kwake, mpira ni kama mfupa wa ziada kwenye mwili wake, na anakimbia na mpira utadhani hayuko nao … Njia pekee ya kumzuia ni kumpiga teke."
 
- Meneja mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Carlos Bilardo akikumbushia falsafa ya Bilardismo.
 
KUANGALIA NJE YA NYUMBA

" IOC? Hawana uwazi! Wana ‘manage’ pesa zao kama vile mke ambaye ni mama wa nyumbani."

- Rais wa FIFA, Sepp Blatter akizungumzia mambo ya nje ya FIFA.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Michel Platini si rafiki wa Mino Raiola, rais huyo Mfaransa wa UEFA ni bosi wa Mafia. Platini hajafanya lolote bora kwa ajili ya manufaa ya soka. Kama angekuwa na uwezo angeibadili UEFA."

- Wakala Mino Raiola akijibu mashambulizi ambayo yatamfurahisha mteja wake nyota, Zlatan.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Takwimu ni kama sketi ‘kimini’, hayaaniki wazi kila kitu."

- Kocha wa Galatasaray, Fatih Terim akielezea mtazamo wake baada ya kuulizwa kuhusu kiwango kibovu cha nyumbani cha timu yake kabla ya mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya CFR Cluj.
 
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Hakuna msamaha katika ubaguzi ... Lakini mashoga hawapaswi kuwamo kwenye timu za soka. Wachezaji wanaoga bila ya nguo pamoja! Nawapenda mashoga, lakini siwezi kumuajiri hata mmoja. Muweke mmoja kwenye timu, hamtashinda mechi tena."

- Mmiliki wa klabu ya Steaua, Gigi Becali akikumbusha kwamba soka ni kwa kila mtu.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Baba yangu alikuwa mkali kuliko Pele ... natumai ataongea nami siku moja."

- Mtoto wa Diego Maradona alisema.
 
NI MTAZAMO TU

"Nikijiunga na Milan itanifungulia milango ya kujiunga na timu kubwa kama Real Madrid na Barca."

- Kiungo mchezesha-timu wa QPR, Adel Taarabt akisema mtazamo wake.
----------------------------------------------------------------------------------------------

"Kuna upinzani wa jadi baina ya Real Madrid na Atletico hivyo nadhani Falcao ni tunda lililokatazwa kuliwa."

- Jose Mourinho akionyesha namna anavyotamani siku moja kumpata mdunguaji wa Kicolombia kwenye timu yake.

----------------------------------------------------------------------------------------------
 
"Arsenal ni timu ambayo inakufanya uote."

- Mshambuliaji wa Newcastle, Demba Ba alisema ya moyoni wakati akijibu kuhusu uvumi wa kutakiwa na Arsenal.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi ya Barcelona."

- Kauli ya Thiago Silva ambaye hata hivyo sasa ametua katika klabu ya PSG.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Ndoto yangu ni kucheza Hispania."

- Nyota wa Anderlecht, Lucas Biglia yeye hakuwa muwazi sana.
 
SITASAHAU

"Waliokufa na walionusurika hawakuumizwa Aprili 15, 1989 mjini Sheffield tu, bali pia kwa miongo zaidi ya miwili mingine kutokana na aibu ya wanaotumia vibaya madaraka na nguvu zao."

- Mahodha wa Liverpool, Steven Gerrard alisema baada ya mwisho wa mwaka baada ya kuona hatua kubwa imepigwa kwa wale ambao hawakukata tama katika kupagania haki za walioathirika katika Janga la Hillsborough.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Nilisema, 'nimeelewa wewe ni mcheza soka mzuri', na akasema 'nitajaribu'."

- Fabrice Muamba anaendelea kuwa na imani kufuatia tukio lake la kuzimia uwanjani White Hart Lane mapema mwaka huu; dunia ina bahati kuwa naye.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Magoli kuanzia leo, nayatoa kwa familia yangu na nawashukuru kwa meseji na sapoti ninayoipata. Pengo aliloacha [baba yangu wa kufikia] halizibiki."

- Ronaldinho akitukumbusha sote kuna mambo muhimu maishani zaidi ya soka, ambayo mchezo wa soka unaweza kutusaidia kuyafidia katika vipindi vigumu.

----------------------------------------------------------------------------------------------

"Niangalie mimi. Nimeshinda taji la ASEAN nikiwa na umri wa miaka 42 … napenda kusema asante kwa Singapore kwa kunipa fursa ya kuchezea timu ya taifa. Ni heshima kubwa."
 
- Aleksandar Duric, bado anapiga soka.

----------------------------------

No comments:

Post a Comment