Sunday, December 30, 2012

'HAT-TRICK' HAITABADILI MSIMAMO WA WALCOTT, ASEMA WENGER

Walcott akiondoka na mpira baada ya kutupia hat-trick
Walcott akiondoka na mpira baada ya kutupia hat-trick
Walcott akishangilia na Olivier Giroud
Giroud akishangilia na Arteta

Giroud akifunga dhidi ya Newcastle

Giroud akifunga goli jingine

Giroud akishangilia goli lake pamoja na Walcott



KOCHA Arsene Wenger amesema kitendo cha Theo Walcott kufunga 'hat-trick' katika ushindi wa 7-3 dhidi ya Newcastle United jana hakitaathiri hatma yake Arsenal.

Mkataba wa sasa wa Walcott unamalizika mwisho wa msimu na atakuwa huru kuzungumza na klabu aipendayo kuanzia wiki ijayo.


Lakini Wenger alisema: "Dhamira yangu ni kumuongeza mkataba. Yeye ni wa hapa na natumai tunaweza kumbakisha.


"Hata kama angecheza soka bovu leo, isingebadili dhamira yangu ya kumuongeza mkataba."


Wenger alisema anaamini Walcott "anaipenda" Arsenal, akiongeza: "Klabu inampenda. Ukubwa wa dhamira yangu (ya kumuongeza mkataba) ni sawa na ilivyokuwa kabla ya mechi.


"Ningependa zaidi kuzungumzia ubora wake wa soka kuliko pesa na uvumi."


Walcott (23) amefunga magoli 14 katika michuano yote msimu huu na magoli manne katika mechi tatu zilizopita tangu alipoanza kuchezwa kama mshambuliaji wa kati.


"Leo imeonyesha kile ambacho nadhani anaweza kukifanya akicheza kama mshambuliaji wa kati," Wenger alisema.


"Goli la kwanza lilikuwa la staili ya Thierry Henry na alionyesha alivyo na 'njaa' ya kufunga katika goli la tatu.
"Amekuwa mmaliziaji mzuri. Amejifunza mengi kwa sababu ni mchezaji mwerevu na kwa sababu ni mwerevu ataongezeka ubora."


Theo Walcott, ambaye amefunga magoli 10 katika mechi 10 zilizopita za Arsenal katika michuano yote, amefunga kwa asilimia 35.8 ya mashuti yake msimu huu katika Ligi Kuu - wastani ambao ni bora kuliko mchezaji yeyote aliyefunga magoli matano au zaidi.

No comments:

Post a Comment