Saturday, December 29, 2012

DI STEFANO AMPIGIA DEBE MOURINHO NA KUTAKA AUNGWE MKONO ZAIDI KUIPA MATAJI REAL MADRID... AWAPOTEZEA PELE, MARADONA, MESSI NA YEYE MWENYEWE KUWA NDIYO BORA KULIKO WOTE KATIKA HISTORIA... BADALA YAKE ATAJA KINA MUNOZ, MORENO

Twende huku mzee...! Mourinho (kulia) akiwa na Di Stefano
Mourinho (kulia) akiwa na Di Stefano

MADRID, HispaniaAlfredo di Stéfano, rais wa heshima wa Real Madrid na straika wa zamani wa mabingwa hao wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania amesema kuwa kura yake bado iko kwa kocha wao José Mourinho: "Ana kibarua kigumu mikononi mwake. Tunapaswa kumuunga mkono na kuendelea kushikamana kwa sababu bado kuna safari ndefu msimu huu".

Di Stéfano pia anaamini kwamba mashabiki wa Real Madrid wanaweza kuwa chanzo cha furaha mwaka ujao: "Real Madrid bado inapigania mataji mawili na ninaamini tutatwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Real Madrid inahitaji kung'oa vikwazo vyote barani Ulaya".

Miongoni mwa mambo aliyotakiwa kuyatolea maoni wakati akizungumza na Marca jana Ijumaa (Desemba 28, 2012) ni jina la mwanasoka bora wa muda wote katika historia, akitakiwa kuchagua miongoni mwa majina ya Pelé, Zico, Platini, Rivelino, Beckenbauer, Maradona, Messi na yeye mwenyewe.

Hata hivyo, jibu lake linaweza kuwashangaza baadhi ya watu: "Siku zote nimekuwa nikifikiria kwamba kuna wakali wengine watano ambao ni wanasoka bora zaidi: "Muñoz, Moreno, Pedernera, Labruna na Loustau".

Muargentina huyo pia alisema wazi kwamba Cristiano Ronaldo ana kura yake katika kuchagua mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA 2012.

Mwisho, alipoulizwa kutaja mwanasoka bora wa enzi zake ambaye angeweza kung'ara katika kizazi cha sasa, Di Stefano alimtaja mchezaji mwenzake kikosini, Francisco Gento, akiongeza kwamba "wengine kadhaa" wangeng'ara pia katika soka la sasa.


No comments:

Post a Comment