Monday, December 10, 2012

MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA KESHO


Michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho (Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.

Viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.

Timu hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.

Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.

Mechi za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2 asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).

Kundi C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)

No comments:

Post a Comment