Monday, December 10, 2012

KATONGO, KALABA, SUNZU WAJA NA CHIPOLOPOLO KUIVAA STARS

Nahodha wa timu ya taifa ya Zambia, Christopher Katongo akilibusu kombe la ubingwa wa Mataifa ya Afrika baada ya kushinda mechi yao ya fainali dhidi ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Stade De L'Amitie katika mji mkuu wa Gabon wa Libreville Februari 12, 2012. Picha: REUTERS

KOCHA wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.

Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.

No comments:

Post a Comment