Wednesday, December 19, 2012

MGOMO WATISHIA MECHI YA ARSENAL v WEST HAM

Uwanja wa Emirates wa klabu ya Arsenal

ARSENAL imesema mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya West Ham iliyopangwa kuchezwa "Boxing Day" iko shakani kutokana na mpango wa mgomo wa wafanyakazi kazi wa treni za ardhini mjini London.

Madereva wa treni za ardhini huenda wakagoma Desemba 26 kutokana na suala la malipo.

Arsenal wamesema wako katika mazungumzo na Kamati ya Kusimamia Ligi Kuu, West Ham, police pamoja na maafisa husika kuhusu uwezekano wa kuahirishwa kwa mechi hiyo.

Mechi za ligi kuu baina ya timu nyingine za London, QPR na Fulham zinatarajiwa kuchezwa kama zilivyopangwa.

Arsenal imesema katika taarifa yake: "Mechi iko shakani kutokana na ugumu wa kupata salama mashabiki 60,000 pamoja na maafisa wote wa mechi na wahudumu wa uwanja kutokana na tatizo la usafiri wa jamii katika siku ya mapumziko.

"Klabu itatoa taarifa zaidi mara maamuzi ya mwisho yatakapofikiwa."

Msimu uliopita, Arsenal walipeleka mbele kwa siku moja mechi yao iliyopaswa kuchezwa wakati wa Boxing Day dhidi ya Wolves kutokana na mgomo kama huo.

No comments:

Post a Comment