Mtuhumiwa mmjojawapo wa tukio la ujambazi uliofanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam leo, Augustino akiwa chini ya ulinzi wa polisi. |
Baadhi ya wananchi wakishangaa katika eneo lililotokea ujambazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2012. |
Dah... ishakuwa noma! |
Wazee wa kazi wakitia timu katika eneo la tukio. |
MIJAMBAZI iliyozua sokomoko kubwa mishale ya asubuhi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam imeua watu wawili wasiokuwa na hatia na pia kufanikiwa kutoroka na fedha taslim Sh. milioni 150, imefahamika.
Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimeeleza kuwa watu waliouawa ni raia wa kawaida, mmoja akilengeshwa mtutu wa bunduki na kupigwa risasi hadi kufa baada ya majambazi kubaini kwamba alikuwa akijaribu kuwadhibiti kwa kuwashambulia kwa mawe huku mwingine akifa baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati akiendelea na shughuli zake za kuuza duka.
Aidha, imefahamika kuwa watu wengine kadhaa walijeruhiwa na majambazi hao ambao walifyatua hovyo risasi kadhaa wakati wakikimbia baada ya kupora fedha zilizokuwa njiani zikisafirishwa kwa gari kutoka katika duka moja la matairi na spea za magari kupelekwa katika tawi moja la Benki ya NMB.
Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema kuwa hadi sasa, watu watatu wametiwa mbaroni wakituhumiwa kwa ujambazi huo, akiwamo mmoja mwenye mwili wa 'kibaunsa' aliyejazia mwili aitwaye Augustino (24). Pia imekamatwa bastola moja ya maujambazi hao.
No comments:
Post a Comment