Tuesday, December 18, 2012

BILIONEA WA PSG AKIRI KUWAFUKUZIA KWA UDI NA UVUMBA JOSE MOURINHO, CRISTIANO RONALDO

Mourinho

Ronaldo
Bilionea Saoud Bin Abdulrahman Al-Thani

Tunatishaaaa....! Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho wa Real Madrid wakishangilia goli
PARIS, Ufaransa
SAOUD Bin Abdulrahman Al-Thani, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Qatar na mtu wa karibu zaidi wa mmiliki wa klabu ya Paris Saint Germain, Sheikh Nasser Al Khelaifi, amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inawafukuzia kwa udi na uvumba straika Cristiano Ronaldo na kocha José Mourinho wa Real Madrid.

"Ni kweli", Saoud Bin Abdulrahman alijibu katika mahojiano yake na kituo cha Canal + France wakati alipoulizwa kama Cristiano Ronaldo na José Mourinho ni miongoni mwa nyota wanaowafukuzia kujiunga na klabu yao hiyo ya jiji la Paris.

"Unapaswa kuwa na hamasa katika dunia ya michezo na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya klabu, kufanya uwekezaji sahihi na katika wakati mwafaka".

Saoud Bin Abdulrahman amesema kuwa hivi sasa, Ibrahimovic ndiye mchezaji wao nyota ("Ni kiongozi wetu") na kwamba matokeo ya klabu yao ya Paris yataimarika katika kila msimu: "Paris Saint Germain ni miongoni mwa klabu bora duninai, nina uhakika na hilo. Tangu mwanzo, lengo letu limekuwa ni kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Sidhani kama hilo ni jambo gumu, sisi ni miongoni mwa klabu bora Ufaransa na tuna matumaini ya kuwa klabu bora Ulaya na hata duniani".

Vyanzo kadhaa vimedai kwamba Paris Saint Germain itakuwa tayari kuipa Real Madrid ofa ya euro milioni 100 (Sh. bilioni 200) kumsajili Cristiano Ronaldo, hivyo kufanya uhamisho wa Mourinho kujiunga katika timu yao kuwa kama umeshakamilika.

No comments:

Post a Comment