Chelsea Frank Lampard (kushoto) akishangilia goli alilofunga
na mwenzake Juan Mata wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwehnye Uwanja
wa Goodison Park mjini Liverpool, leo Desemba 30, 2012. Chelsea imeshinda 2-1. (Picha: REUTERS)
|
Steven Pienaar wa
Everton (kushoto) akichuana na David Luiz wa
Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa
Goodison Park mjini Liverpool, jana. (Picha: REUTERS)
|
LONDON, England
FRANK Lampard alionyesha thamani yake kwa Chelsea baada ya kufunga magoli mawili ‘makali’
yaliyoipa ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Everton leo na kukwea hadi
katika nafasi yake ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Huku kukiwa na uvumi mwingi kuhusiana na hatma yake ndani ya Chelsea,
alionyesha kiwango cha juu na kufunga mabao yote huku goli la Everton
likifungwa na Steven Pienaar.
Ushindi wan ne mfululizo wa Chelsea chini ya kocha Rafael Benitez umeiinua
hadi kubakiza pointi nne tu kabla ya kuifikia Manchester City inayoshika nafasi
ya pili, huku Chelsea ikiwa na mechi moja mkononi.
|
No comments:
Post a Comment