Gooooooooo! Branislav Ivanovic (kulia) wa Chelsea akifunga goli la pili kwa kichwa dhidi ya Leeds jana usiku |
CHELSEA walizinduka kutoka nyuma na kuisambaratisha Leeds kwa mabao 5-1 kwenye uwanja wa Elland Road na kutinga nusu fainali ya Kombe la Ligi (Capital One Cup) jana usiku.
Luciano Becchio alimalizia vyema shambulizi la kustukiza na kuwapa wenyeji uongozi wa 1-0 hadi wakati wa mapumziko pamoja na matumaini ya kupata ushindi maarufu.
Lakini Juan Mata alifunga la kusawazisha dakika mbili baada ya kipindi cha pili kuanza na Branislav Ivanovic akafunga kwa kichwa katika dakika 64 kuiweka Chelsea mbele.
Victor Moses akafunga kwa shuti lililotinga kwenye kona ya chini ya lango kufuatia shambulizi la kustukiza katika dakika ya 66 kabla ya Eden Hazard kufunga la nne katika dakika 85 na Fernando Torres akamalizia kiulaini la tano katika dakika 87 na kuipeleka Chelsea katika hatua ya nusu fainali.
Yalikuwa ni matokeo ambayo yalidumisha rekodi yao ya kutofungwa dhidi ya Leeds katika michuano ya kuwania vikombe na kuwarejesha katika mwendo wao wa kushinda baada ya kufungwa na Corinthians katika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu.
Kwa ushindi huo, Chelsea itaikabili Swansea katika mechi mbili za nusu fainali zitakazochezwa Januari 7 na marudiano Januari 21. Mechi nyingine ya nusu fainali itakayochezwa tarehe hizo hizo itakuwa ni baina ya Bradford iliyoitoa Arsenal dhidi ya Aston Villa.
Vikosi vilikuwa
Leeds United
- 12 Ashdown
- 02 Peltier
- 04 Lees
- 05 Pearce
- 07 Green
- 09 Thomas (White - 68' )
- 17 Brown (Norris - 72' )
- 18 Tonge
- 25 Byram
- 10 Becchio
- 21 El Hadj Diouf (McCormack - 72' )
Wachezaji wa akiba
- 01 Kenny
- 11 Varney
- 14 White
- 19 Norris
- 20 Gray
- 28 Somma
- 44 McCormack
Chelsea
- 01 Cech
- 02 Ivanovic
- 04 David Luiz
- 28 Azpilicueta
- 34 Bertrand (Cole - 74' )
- 08 Lampard
- 10 Mata (Ferreira - 85' )
- 11 Oscar
- 13 Moses
- 21 Marin (Hazard - 60' )
- 09 Torres
Wachezaji wa akiba
- 22 Turnbull
- 03 Cole
- 19 Ferreira
- 17 Hazard
- 56 Saville
- 57 Ake
- 35 Piazon
Refa: Marriner
Mashabiki waliohudhuria: 33,816
No comments:
Post a Comment